Hakuna Marefu Yasiyokuwa Na Ncha

Maisha ni mzunguko, na sisi binadamu tunapoishi hapa duniani, tunakutana na mambo mengi sana yakiwemo mazuri na mengine mabaya, ya kusikitisha na hata yanayofurahisha.

Adui Hatoki Mbali

Usemi huu unatufundisha jinsi tunavyopaswa kuishi na jamii na marafiki wanaotuzunguka. Ni vizuri kuwa karibu na hao watu kwa sababu hata maandiko yamesema binadamu tupendane na tusaidiane. Tunapaswa kujua kuwa hayo yote tunatakiwa tuyafanye kwa kiasi na kwa makini sana. Kumbuka, wema wako unaweza kukupeleka kwenye kilio. Sio kilio cha kufiwa, bali tunaongelea kilio kitokanacho na matatizo utakayoyapata baada ya hapo. 

Usitoe Maamuzi Wakati Una Furaha Sana

Tuko katika ulimwengu wenye vurugu na fujo zisizohesabika. Kila mtu anacho akijuacho ambacho anaona mwingine hakijui na wala hakiwezi. Ni fikira ambazo wanadamu tunatembea nazo. Furaha na huzuni ni sehemu ya maisha yetu.

Mtu Hufurahia Shida Zako, Sio Furaha Yako

Matatizo yameumbwa na kila mtu huyapata. Hakuna mtu ambaye hajawahi kupitia matatizo, na hayuko ambaye hatayapitia. Inategemea ni tatizo gani na wakati gani linakutokea.

Ishi Kadri Unavyojaliwa, Na Sio Kama Mwingine Anavyoishi

Watu wengi wana kawaida ya kupenda kujilinganisha na watu wengine. Watu kama hao hupenda kujiuliza, “kama yule yuko hivi, kwa nini na mimi nisiwe vile?”

Njia Ya Mkato Tamu, Lakini Ina Madhara

Mara nyingi kama mtu anataka afike haraka, anatafuta njia ya kukatisha, njia ya haraka. Njia hiyo inaweza kuwa nzuri pale tu utakapofanikiwa kufika kule uendako. Kuna wakati lakini njia ya mkato inaweza ikakupoteza na ukashindwa kufika uendako. Kuna baadhi ya binadamu, hupenda kutafuta mafanikio kwa kupitia njia ya udanganyifu, kama kutapeli wenzao. 

Ukishindwa Hili Leo, Kesho Utashinda Lile

Wakati sisi tunasoma shule ya msingi, ilikuwa ni madarasa manne tu, yaani la kwanza hadi la nne. Enzi hizo walizingatia sana umuhimu wa kila darasa kuwa na wanafunzi wasiozidi arobaini na tano.