Utaula Wa Chuya Kwa Uvivu Wa Kuchagua

Chuya ni mpunga ambao unakuwa umejichanganya na mchele mzuri ambao upo tayari kwa kupikwa. Hizo chuya huwa zinatakiwa kuchaguliwa ili kupata mchele mzuri, tayari kwa kupikwa. Lakini inawezekana kwa watu wengine ambao ni wavivu, kuupika mchele ukiwa hivyo haujachaguliwa wasione tofauti ama vibaya.

Furaha Ni Kama Marashi Kwani Huongeza Maisha

Wahenga wa kale walisema, “Kitu furaha ni sawasawa na marashi”, kwani huwezi kujipulizia wengine wasisikie harufu yake. Hii inajidhihirisha wazi kwamba ukiwa na furaha huwezi kuificha kwani mtu yeyote atakayekuona atatambua kuwa umefurahi au una furaha. Basi, endapo wewe umefurahi, jitahidi na watu wengine nao wafurahi kutokana na furaha yako.

Usitegemee Uzuri Wako Maana Kuna Siku Utazeeka

Wako mabinti zetu wengi ambao wanajiona ni wazuri kwa umbo na sura. Watu hao mara nyingi hujiona kuwa ni bora zaidi kuliko wengine. Na huwa wanapenda hata kuchagua ni nani watakuwa wenzi wao. 

Wakati Mwingine Hawakupendi, Wanakupenda Kwa Kile Ulicho Nacho

Ni ukweli usiopingika kuwa watu humpenda mtu mwenye nacho. Watu wa aina hii, yaani wale wenye nacho, huwa na marafiki wengi kupita maelezo. Ukweli huu huonekana zaidi kama huyo mtu atakuwa ni mtoaji sana na ambaye anapenda kusaidia watu.

Heri Shetani Unayemjua, Kuliko Malaika Usiyemjua

Tupo duniani tukizungukwa na watu mbalimbali na wenye tabia tofauti tofauti. Tunaishi kwa kutegemeana maana sisi ni wanadamu ndiyo maana utaona watu wanasaidina kwa shida na raha. Zaidi ya hapo utaona kwenye jamii zetu, kuna watu wanaishi kwa kupendana kama ndugu na kufanya vitu pamoja na kushauriana kwa kila jambo linalokuja mbele zao.

Usitumie Usomi Wako Kuwanyanyasa Na Kuwatambia Wenzako

Wako watu wanaojiona, wanaojitapa na kutamba kuwa wana akili sana. Hujiona wamesoma na wameelimika zaidi ya wengine. Watu hawa huchukua fursa hiyo ya kuelimika kama fimbo ya kuwachapia wenzao. Huwanyanyasa wenzao kwani huwaona kuwa ni wajinga na pia hawana elimu. Hali kadhalika, huwadharau, kiasi kwamba hata kuongea nao inakuwa ni shida, kisa, eti hawajasoma.

Mpatie Mtu Ujira Wake Kwa Wakati Anaostahili

Kuna aina nyingi za ajira hapa duniani. Usemi huu unawalenga wale tunaowaajiri hasa kwenye kazi za nyumbani (house girls). Kuna tabia mbaya ya baadhi ya waajiri kwenye sekta hii kutokuwajali na kuwathamini wafanya kazi wa sekta hii.