Maisha Mashenzi

Maisha ni zawadi ambayo Mungu ametupa wanadamu ili tuishi kwa mafanikio kadiri alivyotuahidi maana vyote chini ya jua ni vyetu kwa hiyo kila mtu awe na maisha mazuri na yenye baraka.

Penye Mafanikio Kuna Furaha

Shughuli yoyote ambayo mwanadamu anafanya ni kwa madhumuni ya kufanikiwa. Katika mafanikio hayo ndipo inazaliwa furaha. Daima ukiona mtu amefurahi sana, ukitafuta sababu utakuta kuwa kuna mahali amefanikiwa. Nyumba yeyote ambayo imejaa upendo, basi elewa kuwa pale pana mafanikio kwa njia moja au nyingine.

Heri Lawama Kuliko Fedheha

Lawama ni hali ya kulalamika kuhusu jambo ama tatizo fulani. Fedheha maana yake ni aibu. Mara nyingi watu hutumia muda wao mwingi kulalamikia ugumu wa maisha. Ukiwachunguza watu hao kwa undani utakuta ni wale ambao ni wavivu, wasiopenda kufanya kazi. Mara nyingi watu hao hushinda vijiweni na kuzungumza mambo ya umbea ambayo hayana tija kwao wala kwa jamii. Kati ya watu hawa huwa na dharau na kebehi, wasiotafuta fursa, wasiopenda kushirikiana na wenzao na wenye mtizamo hasi dhidi ya wenzao na wao wenyewe.

Mawazo Ya Watu Wenye Hekima Ni Kama Shamba

Hekima ni mojawapo ya vipaji ambavyo Muumba wetu hutoa kwa viumbe wake. Ieleweke kuwa, sio kila mtu anajaliwa kupata vipaji. Lakini endapo itatokea kuwa unataka kipaji basi unashauriwa kuwa ni vema ukaomba hekima.

Ziba Mwanya Usiruhusu Panya Kupita

Mwanya ni nafasi yoyote ambayo mtu au kitu kinaweza kupita au kupenyeza bila kizuizi. Unaweza kuwa mwanya mkubwa au mwanya mdogo, alimradi hauzuii kilichokusudiwa kupenyeza. Hii ina maana kuwa, jambo lolote linapoanza kuharibika, huanza kidogo kidogo au taratibu sana na wakati mwingine bila hata kutambua.

Mwongo Huwa Hasemi Yake

Mtu mwongo ni yule mtu ambaye anapenda kuongea mambo ya wenzake kwa ushabiki. Mara nyingi huwa anaongea katika mithili ya kumdhalilisha mtu. Watu wa aina hii huwa wana asili ya kuwa na marafiki wengi ambao huvutiwa na stori zake za uongo. Huo ni ubinadamu wa watu ambao hawajitambui. Mara nyingi, kinachofanyika hapo huwa ni unafiki mtupu.

Muda Haumsubiri Mvivu

Kila jambo lina wakati na majira yake. Hata tunapopanga mipango tunaweka na muda wa kutekeleza. Pamoja na hayo, inategemea na jinsi wewe mpangaji wa mipango kama unajali muda na wakati wa kuitekeleza. Usipozingatia utakuta muda umeondoka bila ya matokeo.

Usiogope Kuchukiwa, Ogopa Kulaumiwa

Chuki na lawama ni mambo ambayo yanakuja kwa kasi sana katika maisha ya jamii zetu. Mbaya zaidi, katika mahali pa kazi, hayo yameanza kuwa ndio maisha ya wengi. Kwenye sehemu ya kazi, chuki huja kuhusiana na utendaji wa kazi wa mtu. Kuna ambaye anachukiwa tu kwa sababu ya utendaji wake wa kazi na umakini katika kuitenda kazi aliyokabidhiwa na mkuu wake wa kazi.