Usitumie Usomi Wako Kuwanyanyasa Na Kuwatambia Wenzako

Wako watu wanaojiona, wanaojitapa na kutamba kuwa wana akili sana. Hujiona wamesoma na wameelimika zaidi ya wengine. Watu hawa huchukua fursa hiyo ya kuelimika kama fimbo ya kuwachapia wenzao. Huwanyanyasa wenzao kwani huwaona kuwa ni wajinga na pia hawana elimu. Hali kadhalika, huwadharau, kiasi kwamba hata kuongea nao inakuwa ni shida, kisa, eti hawajasoma.

Mpatie Mtu Ujira Wake Kwa Wakati Anaostahili

Kuna aina nyingi za ajira hapa duniani. Usemi huu unawalenga wale tunaowaajiri hasa kwenye kazi za nyumbani (house girls). Kuna tabia mbaya ya baadhi ya waajiri kwenye sekta hii kutokuwajali na kuwathamini wafanya kazi wa sekta hii.

Usimtekenye Aliyekubeba, Atakudondosha

Maisha yetu ni ya kutegemeana kwa kiwango kikubwa sana. Hakuna mtu atakayesema hapa alipo amefika kwa juhudi zake mwenyewe. Lazima kuna mahali alifika akakwama, na mtu mwingine akamkwamua na hatimaye akatoka.

Cha Mtu Mavi

Tunaishi duniani kwa viwango tofauti vya maisha. Kuna baadhi ya watu wanavyo vitu vya kupitiliza, hadi inakuwa kama kufuru. Wengine wanavyo vya wastani, na wengine wanavyo kidogo au hawana kabisa. Kutokana na hali hiyo wanadamu tunaishi kwa kutoridhika na hivyo tulivyo navyo.

Thamani Ya Mbwa Huisha Mwisho Wa Mawindo

Ni ukweli usiopingika kuwa katika maisha thamani ya mtu huisha pale anapokuwa hayuko tayari tena ama hana uwezo wa kuendelea kutoa msaada. Hii inaweza kutokea kutokana na hali yake kiuchumi kupungua au kutetereka.

Tuache Ukatili Kwa Wanyama, Malipo Ni Hapa Hapa Duniani

Palikuwa na kijana mmoja ambaye alirithi mifugo kutoka kwa baba yake. Hivyo alikuwa mfugaji na mchungaji. Miongoni mwa mifugo aliyorithi, walikuwepo punda, ng’ombe, mbuzi, kondoo, mbwa na kadhalika. Akiwa machungani alikuwa na tabia mbaya ya kuitesa baadhi ya mifugo yake. Moja kati ya wanyama aliyekuwa anateswa sana ni punda ambaye alikuwa anamsadia kubeba mizigo.

Mfungwa Hachagui Gereza

Huo msemo niliujumuisha na usemi ambao tumezoea kuuzungumza. Msemo huo ni ule wa: ‘Sheria ni msumeno ambao unakata kote kote’. Nilishuhudia tukio hili nilipokuwa nasafiri toka Mwanza kuja Dar. Tulipofika Shinyanga tuliona abiria watatu wameingia kwenye basi tulilokuwemo. Mmoja wa abiria hao alikuwa amefungwa pingu.

Tuchukue Tahadhari Stahiki, Dunia Inabadilika Kwa Kasi Mno

Ni ukweli usiopingika kuwa dunia inabadilika kwa kasi kubwa sana kila kukicha, mithili ya mtu aliyegeuza miguu juu, kichwa chini. Dunia ya leo siyo kama ile ya zamani. Dunia ya sasa imekuwa na mambo mengi ya aibu, maovu ya kutisha na ya kusikitisha kiasi kwamba ubinadamu au utu umetoweka. Imefika mahali hatuna huruma tena, tumekuwa kama wanyama. Mambo mengi mabaya yanaibuka kila siku na hata usalama wa binadamu upo mashakani.