Kwa hali yoyote ile,mtu anapotoa sifa nzuri au mbaya kuhusu jambo fulani ni lazima hilo jambo limemkuta na ana uzoefu nalo. Aidha, linaweza likawa limemuathiri kwa ubaya au kwa kufaidika. Hivyo anapolisifia ni kwamba analijua fika kwa undani.
Tag Archives: Swahili Wisdom
Tembo Hachoshwi na Mkonga Wake
Pamoja na uzito wa mkonga wake, tembo huwa hachoki kuubeba popote aendapo. Mkonga wa tembo ni kama matatizo yanayomkuta binadamu katika maisha yake ya kila siku. Matatizo ni sehemu ya maisha, hushitua na kujeruhi mioyo yetu mfano vifo, ajali, magojwa, ndoa, watoto nk. Changamoto tunazopitia kwenye maisha ni kama mkonga wa tembo ambao hauachi, anatembeaContinue reading “Tembo Hachoshwi na Mkonga Wake”
Pole Pole Ndio Mwendo
Umakini wa kufanya mambo unahitajika katika maisha yetu.Tunajifunza kuwa tunapoanza kufanya kitu chochote tusiwe na haraka ya kupata matokeo/mafanikio ya haraka, yatupasa kuwa na subira. Tuepuke kuchukua njia za mkato ambazo zinaweza zisiwe na mafanikio na hatimaye kutupeleka pabaya. Mathalan, ukiwa na biashara au mradi wowote yakupasa uende nao kimkakati ili uweze kupata matunda mazuriContinue reading “Pole Pole Ndio Mwendo”
Asiyesikia la Mkuu Huvunjika Guu
Mtu yeyote mwenye dharau na asiyefuata au kutii maonyo ya wakubwa/waliomzidi umri, mwisho wake huwa ni mbaya. Hivyo, inatupasa kuyasikiliza na kuyafuata maelekezo wanayotupa wakubwa zetu ili maisha yetu yawe ya faida hapa duniani.
Maisha ni Kupanda na Kushuka
Maisha ya mwanadamu yana mapito ya aina mbalimbali, tabu na raha. Changamoto ni moja ya mapito haya, ni sehemu ya maisha yetu wanadamu. Kupitia changamoto tunajifunza mbinu mbali mbali za kupambana na maisha. Changamoto ni msasa wa kusawazisha nyufa za maisha yetu. Tusitishike na changamoto, tusikate tamaa tunapopata majaribu. Tunatakiwa kuzikubali na kusonga mbele. HataContinue reading “Maisha ni Kupanda na Kushuka”
Mvumilivu Hula Mbivu
Tunajifunza umuhimu wa kuwa wavumilivu katika maisha yetu haijalishi tunapitia mazingira magumu kiasi gani. Maisha yana mapito mengi, yatupasa kutulia na kufanya maamuzi ya busara ili hatimaye tuweze kupata malipo ya uvumilivu wetu. Hata kama maisha tunayoishi hayatupatii yale tunayoyategemea, yatupasa kuendelea kuamini kuwa iko siku tutafanikiwa. Hakuna kisichowezekana chini ya jua.
Dalili za Mvua ni Mawingu!
Kabla jambo lolote halijatokea huwa kuna dalili zinazotangulia kuashiria matukio fulani. Dalili hizo zikijitokeza humuandaa muhusika kujiweka tayari kulipokea jambo litakalotokea kwa umakini zaidi.
Baada ya Dhiki Faraja
Tunakumbushwa kuwa kila wakati mgumu ambao mtu anapitia utapita na baadaye utakuja wakati wa raha ambao utamfanya kusahau magumu yote aliyopitia. Inasemekana kuwa mara nyingi magumu tunayopitia ni dalili ya kupata faraja huko mbele. Tunafundishwa kutokata tamaa kutokana na magumu tupitiayo badala yake tufanye kazi kwa bidii katika mazingira yoyote kwani baadaye matunda mazuri yataonekana
Pilipili Usizozila Zakuwashia Nini?
Ni fundisho kwa wale wanaopenda kuwachunguza wenzao kwa mambo ambayo hayawahusu hasa wambea wenye tabia za kuchonganisha watu kwenye jamii, leo atachukua la Hadija atampelekea Zuena kesho anachukua la Maria atampelekea Subira.
Mgaagaa na Upwa Hali Wali Mkavu
Mtu yeyote anayehangaika na shughuli mbali mbali au mtu mwenye bidii za kazi huwa hakosi mafanikio au matokeo mazuri, hupata riziki, mafanikio/matokeo mazuri ambayo humfariji na hali kadhalika huyafurahia hapo mbeleni.