Mvumilivu Hula Mbivu

Tunajifunza umuhimu wa kuwa wavumilivu katika maisha yetu haijalishi tunapitia mazingira magumu kiasi gani. Maisha yana mapito mengi, yatupasa kutulia na kufanya maamuzi ya busara ili hatimaye tuweze kupata malipo ya uvumilivu wetu. Hata kama maisha tunayoishi hayatupatii yale tunayoyategemea, yatupasa kuendelea kuamini kuwa iko siku tutafanikiwa. Hakuna kisichowezekana chini ya jua.

Baada ya Dhiki Faraja

Tunakumbushwa kuwa kila wakati mgumu ambao mtu anapitia utapita na baadaye utakuja wakati wa raha ambao utamfanya kusahau magumu yote aliyopitia. Inasemekana kuwa mara nyingi magumu tunayopitia ni dalili ya kupata faraja huko mbele. Tunafundishwa kutokata tamaa kutokana na magumu tupitiayo badala yake tufanye kazi kwa bidii katika mazingira yoyote kwani baadaye matunda mazuri yataonekana

Haba na Haba Hujaza Kibaba

Usikate tamaa unapoanza na kidogo ulichonacho hicho ndiyo kitakuwa ufunguo wa mafanikio yako. Kwa mfano unaanza biashara na pesa kidogo mathalan shilingi elfu ishirini, usiidharau, hiyo hiyo elfu ishirini uliyoanza nayo baada ya mwezi mmoja unaweza kujikuta una laki moja. Tuwe na moyo wa subira na moyo wa kuthubutu. Pia msemo huu unafanana na uleContinue reading “Haba na Haba Hujaza Kibaba”

Simba Mwenda Pole Ndie Mla Nyama

Tuaona simba awindapo anakuwa makini na anatumia juhudi na maarifa ili apate mawindo yake. Hii ina maana kuwa katika maisha lazima uwe na malengo na si hivyo tu, ili kufanikiwa ni lazima uwe na juhudi na umakini mwingi unahitajika. Inabidi utumie busara na maarifa katika kuyafikia malengo yako. Ukizingatia hayo, utafanikiwa, tuache uvivu.