Neno yatima au ukiambiwa yule ni yatima kila mtu ataelewa. Yatima ni mtoto ambaye, aidha kafiwa na mzazi mmoja au kafiwa na wazazi wake wote wawili.
Tag Archives: Swahili Wisdom
Usimtekenye Aliyekubeba, Atakudondosha
Maisha yetu ni ya kutegemeana kwa kiwango kikubwa sana. Hakuna mtu atakayesema hapa alipo amefika kwa juhudi zake mwenyewe. Lazima kuna mahali alifika akakwama, na mtu mwingine akamkwamua na hatimaye akatoka.
Barua Ya Moyo Husomwa Kwenye Paji La Uso
Moyo ni kitu kidogo sana katika mwili wa mwanadamu. Moyo huwa hauonekani kwa jicho la kawaida, lakini moyo ndio uhai wa mtu ulipo.
Cha Mtu Mavi
Tunaishi duniani kwa viwango tofauti vya maisha. Kuna baadhi ya watu wanavyo vitu vya kupitiliza, hadi inakuwa kama kufuru. Wengine wanavyo vya wastani, na wengine wanavyo kidogo au hawana kabisa. Kutokana na hali hiyo wanadamu tunaishi kwa kutoridhika na hivyo tulivyo navyo.
Thamani Ya Mbwa Huisha Mwisho Wa Mawindo
Ni ukweli usiopingika kuwa katika maisha thamani ya mtu huisha pale anapokuwa hayuko tayari tena ama hana uwezo wa kuendelea kutoa msaada. Hii inaweza kutokea kutokana na hali yake kiuchumi kupungua au kutetereka.
Tuache Ukatili Kwa Wanyama, Malipo Ni Hapa Hapa Duniani
Palikuwa na kijana mmoja ambaye alirithi mifugo kutoka kwa baba yake. Hivyo alikuwa mfugaji na mchungaji. Miongoni mwa mifugo aliyorithi, walikuwepo punda, ng’ombe, mbuzi, kondoo, mbwa na kadhalika. Akiwa machungani alikuwa na tabia mbaya ya kuitesa baadhi ya mifugo yake. Moja kati ya wanyama aliyekuwa anateswa sana ni punda ambaye alikuwa anamsadia kubeba mizigo.
Mfungwa Hachagui Gereza
Huo msemo niliujumuisha na usemi ambao tumezoea kuuzungumza. Msemo huo ni ule wa: ‘Sheria ni msumeno ambao unakata kote kote’. Nilishuhudia tukio hili nilipokuwa nasafiri toka Mwanza kuja Dar. Tulipofika Shinyanga tuliona abiria watatu wameingia kwenye basi tulilokuwemo. Mmoja wa abiria hao alikuwa amefungwa pingu.
Tuchukue Tahadhari Stahiki, Dunia Inabadilika Kwa Kasi Mno
Ni ukweli usiopingika kuwa dunia inabadilika kwa kasi kubwa sana kila kukicha, mithili ya mtu aliyegeuza miguu juu, kichwa chini. Dunia ya leo siyo kama ile ya zamani. Dunia ya sasa imekuwa na mambo mengi ya aibu, maovu ya kutisha na ya kusikitisha kiasi kwamba ubinadamu au utu umetoweka. Imefika mahali hatuna huruma tena, tumekuwa kama wanyama. Mambo mengi mabaya yanaibuka kila siku na hata usalama wa binadamu upo mashakani.
Maisha Mashenzi
Maisha ni zawadi ambayo Mungu ametupa wanadamu ili tuishi kwa mafanikio kadiri alivyotuahidi maana vyote chini ya jua ni vyetu kwa hiyo kila mtu awe na maisha mazuri na yenye baraka.
Penye Mafanikio Kuna Furaha
Shughuli yoyote ambayo mwanadamu anafanya ni kwa madhumuni ya kufanikiwa. Katika mafanikio hayo ndipo inazaliwa furaha. Daima ukiona mtu amefurahi sana, ukitafuta sababu utakuta kuwa kuna mahali amefanikiwa. Nyumba yeyote ambayo imejaa upendo, basi elewa kuwa pale pana mafanikio kwa njia moja au nyingine.