Chovya Chovya Humaliza Buyu La Asali

Maisha ni Kupanda na Kushuka

Maisha ya mwanadamu yana mapito ya aina mbalimbali, tabu na raha. Changamoto ni moja ya mapito haya, ni sehemu ya maisha yetu wanadamu. Kupitia changamoto tunajifunza mbinu mbali mbali za kupambana na maisha. Changamoto ni msasa wa kusawazisha nyufa za maisha yetu. Tusitishike na changamoto, tusikate tamaa tunapopata majaribu. Tunatakiwa kuzikubali na kusonga mbele. HataContinue reading “Maisha ni Kupanda na Kushuka”

Mvumilivu Hula Mbivu

Tunajifunza umuhimu wa kuwa wavumilivu katika maisha yetu haijalishi tunapitia mazingira magumu kiasi gani. Maisha yana mapito mengi, yatupasa kutulia na kufanya maamuzi ya busara ili hatimaye tuweze kupata malipo ya uvumilivu wetu. Hata kama maisha tunayoishi hayatupatii yale tunayoyategemea, yatupasa kuendelea kuamini kuwa iko siku tutafanikiwa. Hakuna kisichowezekana chini ya jua.

Baada ya Dhiki Faraja

Tunakumbushwa kuwa kila wakati mgumu ambao mtu anapitia utapita na baadaye utakuja wakati wa raha ambao utamfanya kusahau magumu yote aliyopitia. Inasemekana kuwa mara nyingi magumu tunayopitia ni dalili ya kupata faraja huko mbele. Tunafundishwa kutokata tamaa kutokana na magumu tupitiayo badala yake tufanye kazi kwa bidii katika mazingira yoyote kwani baadaye matunda mazuri yataonekana

Haba na Haba Hujaza Kibaba

Usikate tamaa unapoanza na kidogo ulichonacho hicho ndiyo kitakuwa ufunguo wa mafanikio yako. Kwa mfano unaanza biashara na pesa kidogo mathalan shilingi elfu ishirini, usiidharau, hiyo hiyo elfu ishirini uliyoanza nayo baada ya mwezi mmoja unaweza kujikuta una laki moja. Tuwe na moyo wa subira na moyo wa kuthubutu. Pia msemo huu unafanana na uleContinue reading “Haba na Haba Hujaza Kibaba”