Pilipili Usizozila Zakuwashia Nini?

Ni fundisho kwa wale wanaopenda kuwachunguza wenzao kwa mambo ambayo hayawahusu hasa wambea wenye tabia za kuchonganisha watu kwenye jamii, leo atachukua la Hadija atampelekea Zuena kesho anachukua la Maria atampelekea Subira.

Haba na Haba Hujaza Kibaba

Usikate tamaa unapoanza na kidogo ulichonacho hicho ndiyo kitakuwa ufunguo wa mafanikio yako. Kwa mfano unaanza biashara na pesa kidogo mathalan shilingi elfu ishirini, usiidharau, hiyo hiyo elfu ishirini uliyoanza nayo baada ya mwezi mmoja unaweza kujikuta una laki moja. Tuwe na moyo wa subira na moyo wa kuthubutu. Pia msemo huu unafanana na uleContinue reading “Haba na Haba Hujaza Kibaba”

Simba Mwenda Pole Ndie Mla Nyama

Tuaona simba awindapo anakuwa makini na anatumia juhudi na maarifa ili apate mawindo yake. Hii ina maana kuwa katika maisha lazima uwe na malengo na si hivyo tu, ili kufanikiwa ni lazima uwe na juhudi na umakini mwingi unahitajika. Inabidi utumie busara na maarifa katika kuyafikia malengo yako. Ukizingatia hayo, utafanikiwa, tuache uvivu.

BUSARA ZIANGUKIAZO KWENYE “T” TATU

Mama Sixtha Komba anatueleza juu ya T tatu ambazo unaweza tumia katika kuyakabili matatizo ukutananayo. Akianza na fafanuzi juu ya T tatu. T1 ni Tatizo T2 ni Tatuzi T3 ni Tokeo Mama Sixtha Komba anaendelea kufafanua hizi T tatu katika nyanja mbili, hasi na chanya kwa kutumia mfano wa mwanafunzi aliyefeli mitihani yake na jinsiContinue reading “BUSARA ZIANGUKIAZO KWENYE “T” TATU”