Kazi ndio msingi wa maisha. Binadamu sote hujishughulisha na kazi ili waweze kuishi. Katika mchakato huo wa kufanya kazi, unakutana na watu wengi ambao nyote mpo kwa ajili ya kufanya kazi na kupata riziki
Tag Archives: Msongo wa mawazo
Mchumia Juani Hulia Kivulini
Mchumia juani ni mtu anayetafuta riziki kwa kufanya kazi, biashara au ujasiriamali. Jitihada hizo hufanywa kwa bidii. Kulia kivulini ni mafanikio au matunda anayopata baada ya kazi ngumu
Kawia Ufike
Kukawia ni kuchelewa au kutofika kwa wakati unaotakiwa. Wanaposema kawia ufike wana maana chelewa lakini ufike mahali unapotakiwa kuwa. Msemo huu unatumiwa sana na baadhi ya watu wasiojitambua na wasiokuwa na uhakika wanatakiwa wafanye nini. Sehemu za ibada ni moja za sehemu ambazo watu hutumia sana msemo huu. Wanapoutumia msemo huu kwenye masuala ya nyumba za ibada, wanakuwa na maana kuwa hata wakikawia, ili mradi watakuwa wamefika, haijalishi sana. Kwa wanaosema hivi ina maana kuwa, cha muhimu kwao ni kuonekana kuwa walikuwepo ili mradi wasieleweke vibaya
Mwamini Mungu Si Mtovu
Alikuweko mtu mmoja na mkewe, hawakuwa na kitu, rasilimali yao kubwa ilikuwa ni kondoo na jogoo. Siku moja walipata habari kuwa rafiki yao alikuwa anakuja kuwatembelea. Mke alimwambia mume wake kuhusu ugeni huo. Alimkumhusha kwa kusema kuwa walikuwa hawana kitu chochote cha kumkirimu mgeni wao. Walichokuwa nacho ni huyo kondoo na jogoo. Lakini, mke aliongeza kuwa yeye asingependa kuwachinja wanyama wake, yaani kondoo jogoo
Kaa Mbali Na Mazoea
Maisha yetu katika ulimwengu huu ni ya vurugu kati ya mtu na mtu. Chochote mtu akifanyacho kimeanzia kwenye fikra zake. Kwa kawaida, mtu hawezi kukurupuka tu na kuanzisha kitu bila kufikiria na kupembua kama hilo jambo litawezekana ama la. Mara nyingi, tunafanya kosa kumshirikisha mtu ama watu mawazo yetu mapema mno. Inawezekana, huyo unayemshirikisha hawezi kukutia moyo ili ufanikiwe, binadamu wengi ndivyo walivyo. Wengi hupenda kukatisha tamaa wenzao na hata kunena maneno mengi ambayo yanaweza kukutoa kwenye wazo lako.
Fikra Zako Usimshirikishe Mtu
Maisha yetu katika ulimwengu huu ni ya vurugu kati ya mtu na mtu. Chochote mtu akifanyacho kimeanzia kwenye fikra zake. Kwa kawaida, mtu hawezi kukurupuka tu na kuanzisha kitu bila kufikiria na kupembua kama hilo jambo litawezekana ama la. Mara nyingi, tunafanya kosa kumshirikisha mtu ama watu mawazo yetu mapema mno. Inawezekana, huyo unayemshirikisha hawezi kukutia moyo ili ufanikiwe, binadamu wengi ndivyo walivyo. Wengi hupenda kukatisha tamaa wenzao na hata kunena maneno mengi ambayo yanaweza kukutoa kwenye wazo lako.
Elimu Bila Vitendo Ni Sawa Na Bure
Elimu ni maarifa anayopata mtu darasani. Vijana wengi wamepata elimu wakianzia chekechea hadi vyuo . Baadhi yao elimu hiyo imewasaidia, wakafanikiwa na wengine kwa bahati mbaya walishindwa
Binadamu Ana Nyuso Mbili, Kaa Nae Kwa Akili
Mara nyingi tumeona kuwa siyo watu wote wanaokuzunguka ni wema kwako. Wewe unaweza ukajiona kuwa ni mwema kwa watu na wao , vivyo hivyo, ukawaona ni wema kwako. Katika imani hiyo unaweza ukajiridhisha na kuona kuwa una ndugu au marafiki wa haja, marafiki wa kukimbiliwa ukiwa na shida.
Kisa Cha Kuku Na Kanga
Hapo zamani kuku walikuwa ndege wa mwituni. Waliishi pamoja na kanga na ndege wengine. Basi siku moja ikaja mvua kubwa huko mwituni. Kanga akamwambia kuku, nenda kwa binadamu ukaombe moto ili tuje tuote. Baridi imezidi, ni kali sana. Kuku alitii agizo la kanga. Alienda, na alipofika kwa binadamu, alikaribishwa vizuri. Binadamu alimuuliza shida iliyompeleka hapo.