Tag Archives: Afya ya akili
Kushinda na Kushindwa ni Sehemu ya Maisha ya Binadamu
Kikulacho Ki Nguoni Mwako
Ukiinuliwa Tulizana
Mdharau Mwiba Guu Huota Tende
Hujafa Hujaumbika
Bandu Bandu Humaliza / Huisha Gogo
Yatupasa tujitume kwa bidii ili kupunguza kidogo kidogo kazi zetu hata kama ni kubwa kiasi gani. Haifai kutanguliza malalmiko. Kuwa na subira katika utekelezaji wa kazi zako, utashtukia umekamilisha kazi zako zote bila kutegemea.
Aisifuye Mvua Imemnyea
Kwa hali yoyote ile,mtu anapotoa sifa nzuri au mbaya kuhusu jambo fulani ni lazima hilo jambo limemkuta na ana uzoefu nalo. Aidha, linaweza likawa limemuathiri kwa ubaya au kwa kufaidika. Hivyo anapolisifia ni kwamba analijua fika kwa undani.
Tembo Hachoshwi na Mkonga Wake
Pamoja na uzito wa mkonga wake, tembo huwa hachoki kuubeba popote aendapo. Mkonga wa tembo ni kama matatizo yanayomkuta binadamu katika maisha yake ya kila siku. Matatizo ni sehemu ya maisha, hushitua na kujeruhi mioyo yetu mfano vifo, ajali, magojwa, ndoa, watoto nk. Changamoto tunazopitia kwenye maisha ni kama mkonga wa tembo ambao hauachi, anatembeaContinue reading “Tembo Hachoshwi na Mkonga Wake”
Pole Pole Ndio Mwendo
Umakini wa kufanya mambo unahitajika katika maisha yetu.Tunajifunza kuwa tunapoanza kufanya kitu chochote tusiwe na haraka ya kupata matokeo/mafanikio ya haraka, yatupasa kuwa na subira. Tuepuke kuchukua njia za mkato ambazo zinaweza zisiwe na mafanikio na hatimaye kutupeleka pabaya. Mathalan, ukiwa na biashara au mradi wowote yakupasa uende nao kimkakati ili uweze kupata matunda mazuriContinue reading “Pole Pole Ndio Mwendo”