Yatupasa tujitume kwa bidii ili kupunguza kidogo kidogo kazi zetu hata kama ni kubwa kiasi gani. Haifai kutanguliza malalmiko. Kuwa na subira katika utekelezaji wa kazi zako, utashtukia umekamilisha kazi zako zote bila kutegemea.
Tag Archives: Afya ya akili
Aisifuye Mvua Imemnyea
Kwa hali yoyote ile,mtu anapotoa sifa nzuri au mbaya kuhusu jambo fulani ni lazima hilo jambo limemkuta na ana uzoefu nalo. Aidha, linaweza likawa limemuathiri kwa ubaya au kwa kufaidika. Hivyo anapolisifia ni kwamba analijua fika kwa undani.
Tembo Hachoshwi na Mkonga Wake
Pamoja na uzito wa mkonga wake, tembo huwa hachoki kuubeba popote aendapo. Mkonga wa tembo ni kama matatizo yanayomkuta binadamu katika maisha yake ya kila siku. Matatizo ni sehemu ya maisha, hushitua na kujeruhi mioyo yetu mfano vifo, ajali, magojwa, ndoa, watoto nk. Changamoto tunazopitia kwenye maisha ni kama mkonga wa tembo ambao hauachi, anatembeaContinue reading “Tembo Hachoshwi na Mkonga Wake”
Pole Pole Ndio Mwendo
Umakini wa kufanya mambo unahitajika katika maisha yetu.Tunajifunza kuwa tunapoanza kufanya kitu chochote tusiwe na haraka ya kupata matokeo/mafanikio ya haraka, yatupasa kuwa na subira. Tuepuke kuchukua njia za mkato ambazo zinaweza zisiwe na mafanikio na hatimaye kutupeleka pabaya. Mathalan, ukiwa na biashara au mradi wowote yakupasa uende nao kimkakati ili uweze kupata matunda mazuriContinue reading “Pole Pole Ndio Mwendo”
Asiyesikia la Mkuu Huvunjika Guu
Mtu yeyote mwenye dharau na asiyefuata au kutii maonyo ya wakubwa/waliomzidi umri, mwisho wake huwa ni mbaya. Hivyo, inatupasa kuyasikiliza na kuyafuata maelekezo wanayotupa wakubwa zetu ili maisha yetu yawe ya faida hapa duniani.
MAHUSIANO MAZURI YANAYO RUHUSU MAJADILIANO
Mama Sixtha Komba (M&E Officer, TEWWY) atuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na uwanja wa majadiliano hasa kati ya vizazi.
BUSARA ZIANGUKIAZO KWENYE “T” TATU
Mama Sixtha Komba anatueleza juu ya T tatu ambazo unaweza tumia katika kuyakabili matatizo ukutananayo. Akianza na fafanuzi juu ya T tatu. T1 ni Tatizo T2 ni Tatuzi T3 ni Tokeo Mama Sixtha Komba anaendelea kufafanua hizi T tatu katika nyanja mbili, hasi na chanya kwa kutumia mfano wa mwanafunzi aliyefeli mitihani yake na jinsiContinue reading “BUSARA ZIANGUKIAZO KWENYE “T” TATU”