Aanguaye Huanguliwa

Masimulizi …

by Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY).

Mara nyingi binadamu hupenda kutendea wenzao mambo ambayo wao hawapendi kutendewa. Mathalan, mtu anaweza akawa na cheo kikubwa kwenye kampuni, serikali ama shirika lisilo la kiserikali. Katika madaraka yake hayo akawa ni mtu wa vitisho sana na unyayasaji kwa watu wa chini anaowaongoza. Tabia hii ya vitisho na unyanyasaji hukithiri hadi kufikia kuanza kuwafukuza watu na kuwaacha bila kazi.

Familia za walioachishwa kazi hubaki nyuma katika mashaka makubwa na hatimaye hukosa mahitaji yao muhimu. Mateso na masumbuko ya familia hizo huja kulipwa hatimaye. Jamaa ambaye ni bosi mdogo naye ana bosi wakubwa waliomzidi cheo. Katika utendaji wake wa kazi naye pia anaweza akapatikana na makosa na hatimaye akaenguliwa. Yatupasa kupendana na kusaidiana kuliko kuwatafutia makosa ama visa wenzetu kwa sababu tu tuna vyeo na tunataka kutunishiana misuli. Watu husema, ‘malipo ni hapa hapa duniani’. Tufuate taratibu za kiutu na kibinadamu, yasije yakatukuta hayo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Tabia Nzuri Yamnusuru Kifo

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi …

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Tabia njema siku zote ni kinga au akiba dhidi ya mambo mabaya yanayoweza kukutokea katika maisha yako baadaye. Katika kuthibitisha hilo, tuone ni jinsi gani msemo huo unavyoweza kuwa na ukweli kama ifuatavyo:

Kulikuwa na baba mmoja ambaye alifanya kazi katika kiwanda cha barafu. Kila siku asubuhi alipokuwa akiingia kazini alikuwa na tabia ya kumsalimu mlinzi wa pale getini. Vivyo hivyo jioni anapotoka alimuaga mlinzi na kuondoka kwenda nyumbani.

Siku moja jioni wafanyakazi wakiwa wanajiandaa kuondoka kurudi makwao, kiwandani kulitokea tatizo ambalo ilibidi yule baba arudi pale kiwandani ili kulishughulikia. Alipomaliza, ghafla umeme ulikatika, milango yote ikajifunga na haikuweza kufunguka. Kwa kuwa kulikuwa hakuna mawasiliano mle ndani, baba huyu alinasa ndani, akashindwa kutoka. Kwa bahati nzuri mfanyakazi huyo alikuwa na tabia nzuri iliyoambatana na mazoea ya kumsalimia mlinzi kila siku asubuhi anapoingia na kumuaga kila siku aondokapo jioni. Kutokana na hali hii, alipokwama ilikuwa rahisi kwa mlinzi kutambua kuwa yule mfanyakazi alikuwa bado hajatoka kwa sababu ilikuwa bado hajamuaga.

Hali hiyo ya kutokumuona yule
baba ilimshitua sana mlinzi. Alianza kuzunguka kiwandani kote kumtafuta na hatimaye alipogundua kuwa umeme ulikuwa umekatika alijua kuwa alikuwa amenasa mle ndani ya kiwanda. Kwa haraka alivunja mlango ili amuokoe yule baba.
Alimpata akiwa bado hai ingawa alikuwa dhaifu sana.

Alimpeleka hospitali ambako alilazwa kwa matibabu. Baada ya siku chache alipona na akarudi nyumbani na hatimaye kurejea kazini akiwa na afya njema.

Kisa hiki kinatufundisha kuwa kila siku katika maisha yetu yatupasa kutenda angalau jambo moja jema, kama kusalimiana na wenzetu kama alivyokuwa akifanya huyu baba. Kwake yeye, utu wake ulikuwa ni akiba ya ukombozi wake wakati alipokuwa amenaswa kwenye kiwanda cha barafu.
Funzo hili linalandana na methali zifuatazo: ‘Wema hauozi, na Akiba haiozi.’

Tujifunze kuwekeza mema kwa faida za baadaye.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Usiwaze Yaliyopita Au Ya Zamani, Yatakuchelewesha

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi …

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha yetu tunapitia mazuri na mabaya. Mara nyingi wengi wetu tuna tabia ya kuyakumbuka na kuyatafakari mabaya yaliyopita, lakini hiyo haisaidii lolote zaidi ya kutuongezea machungu na maumivu. Kama wana falsafa wasemavyo, maji yakimwagika hayazoleki, ni kweli kabisa, hata ungekuwa na utaalamu wa namna gani huwezi ukayazoa. Kwa hiyo hatupaswi kuendelea kuruhusu kuwaza makosa tuliyowahi kuyatenda katika maisha yetu ya huko nyuma. Kwa mfano mtu unajikuta unasema laiti ningelijua tangu mwanzo nisingekubali au nisingefanya hayo niliyoyatenda. Maneno yanayoanza na … ningelijua… nisinge… huwa Haya a maana katika maisha ya mwanadamu. Tujifunze kuyafuta na kuyasahau kabisa makosa yetu ya zamani kwa lengo la kuyatazama mema na mazuri yaliyoko mbele yetu. Tuchukue hatua sahihi za kutufikisha pazuri. BUSARA zetu zitusaidie kutumia makosa tuliyowahi kuyafanya kama sehemu ya kujifunza na kutoruhusu makosa mengine tena ili kutengeneza maisha mapya na kuweza kusonga mbele.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Chovya Chovya Humaliza Buyu La Asali

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi …

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha yatupasa kufanya kazi zetu kwa umakini, uangalifu na utaratibu sahihi. Unaweza ukawa na kazi kubwa sana mbele yako na pengine ikakutisha tamaa na kuona kuna uwezezekano mdogo wa kuimaliza. Unachotakiwa kufanya ni kuipunguza kazi hiyo kidogo kidogo na hatimaye unaweza ukaimaliza. Tunaweza tukaifananisja busara hii na msemo wa “pole pole ndio mwendo”. Utendaji wa shughuli kwa mpangilio uliojiwekea utakupa matokeo chanya na kuondoa woga na mashaka uliyokuwa nayo mwanzoni kabla ya kuanza utekelezaji wake. Kwenye mchakato huo tunapata uzoefu ambao utatusaidia kuleta matokeo chanya kwenye shughuli yetu nzima. Kwa kuzingatia hayo tunaweza kumaliza kazi iliyokuwa inatutisha kwa ukubwa wake na kuleta mashaka ya kuimaliza, bila kujichosha na hali kadhalika, kwa umakini mkubwa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Rafiki Mwaminifu Na Wa Kweli Ni Yupi?

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi …

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika nchi moja ya ughaibuni alitokea Mfalme mmoja ambaye alioa wake wanne. Siku moja Mfalme aliugua kiasi kwamba alijiona anakufa, akaogopa upweke huko ahera.

Ilibidi awaulize wake zake swali moja lakini kila moja kwa wakati tofauti. Alianza na mke wa nne ambaye alikuwa anampenda sana, kupita wake zake wengine wote. Mke huyu alikuwa anamununulia vito vingi na vya thamani sana.

Mfalme alianza:
Mke wangu mpenzi, je nikifa leo uko tayari kufa nami na kufuatana nami ahera?

Mke wa nne alijibu:
“Samahani, haiwezekani hata kidogo, siwezi kufuatana nawe”, akaondoka zake.

Majibu ya mke wa tatu hayakuwa tofauti sana na yale ya mke wa nne, kwani alisema:
“Mimi ninayapenda sana maisha yangu, sitaweza kwenda nawe, ila itanipasa niolewe na mtu mwingine”.

Majibu ya mke wa pili yalikuwa hivi:
“Siwezi kwenda nawe ila nitakuandalia mazishi na nitayasimamia vizuri hadi mwisho, lakini sitafuatana nawe”.

Wakati anamjibu hivyo, ilisikika sauti ikisema:
“Nitaishi nawe milele katika raha na shida, hata kama ni maisha baada ya kufa”.

Mfalme aligundua kuwa aliyekuwa anaongea ni mke wake wa kwanza ambaye alikuwa hamjali wala kumtunza wakati akiwa na nguvu zake. Baada ya kutambua makosa yake, Mfalme alimwomba mke wake wa kwanza msamaha kwa kutomjali wala kumtunza kwa muda wote alioishi naye.

Mazungumzo haya yanatufundisha kuwa, kila binadamu ana wake wanne. Mke wa nne ni MWILI ambao huwa tunaugharamia na kuupamba kwa vito vya thamani na nguo za gharama kubwa lakini baada ya kufa hatufuatani na mwili huo.

Mke wa tatu ni MALI zetu ambazo tunajikusanyia kwa wingi lakini siku ya mwisho hatuwezi kufuatana nazo. Mali zote huwa zinaachwa na kugawiwa kwa ndugu wanaobaki. Hii ni sawasawa na mke wa tatu alivyosema kuwa ataolewa na mtu mwingine.

Mke wa pili anafananishwa na marafiki na familia zetu. Hawa watu huwa tunawathamini, tunawaamini na kuwapenda sana lakini nao pia hawawezi kwenda nasi zaidi ya kufika makaburini.

Mke wa kwanza ni ROHO zetu ambazo mara nyingi hatuzitilii maanani wala kuzijali. Roho ndizo pekee ambazo zitatufuata hata baada ya kufa.

Kwa hiyo tunaaswa kuijali miili yetu ili iwe na afya njema, kufurahia na kufaidi mali zetu tungali hai. Hali kadhalika, tuwathamini na kuwafurahia marafiki na familia zetu kwa upendo wanaotupa. Pamoja na hayo yote tukumbuke pia kutunza roho zetu kwa sababu roho ni chanzo cha maisha yetu na rafliki mwaminifu na wa ukweli.

Hata hivyo kuwa na marafiki wengi si hoja, hoja ni kuweza kuwachambua na kuwamudu. Hapa duniani tunapita na kila moja ataenda peke yake siku zake zikifika.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. . Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #ArtTherapy #Tanzania

Mtaka Yote Kwa Pupa Hukosa Yote

Masimulizi …

by Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY).

Watu wasiokuwa na misimamo thabiti ya maisha, watu wenye tamaa, watu wanaopenda kushiriki katika mambo ambayo ni makubwa kupita uwezo wao huishia pabaya kwa sababu ya tamaa. Watu hawa hupenda kushika hiki mara kile bila mafanikio. Tuchukue mfano wa vijana wanaotafuta ajira kwenye makampuni ama mashirika fulani. Akienda huku anaona hakufai, akienda kule anaona hakufai, badala ya kutulia mahali pamoja na kuangalia ataendeleaje mahali hapo anarukia sehemu nyingine. Huko kuruka ruka kwake kunamsababishia mwisho wa siku kukosa sehemu zote. Katika maisha yatupasa kuwa na subira, tamaa ni mbaya, pupa ni mbaya. Tuzingatie mambo tunayoyafanya na kufanya maamuzi ya busara ili mwisho wa siku tusikose yote.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. . Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #ArtTherapy #Tanzania

Sikio la Kufa Halisikii Dawa

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi …

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Siku zote yeyote asiyesikia analoambiwa na wakubwa zake huishia pabaya. Mtoto mmoja tangu akiwa mdogo alianza tabia ya udokozi akiwa nyumbani kwao. Wazazi walimkanya lakini hakusikia. Aliendelea na tabia hiyo ya wizi kwa majirani na shuleni, alikanywa na waalimu wake, napo pia hakusikia. Alipomaliza darasa la saba alifaulu lakini akachagua kuendelea na tabia yake ya wizi. Aliamua kujiunga na makundi mabaya, makundi ya majambazi wenye uzoefu. Siku moja walienda kuiba benki, kwa bahati mbaya yule kijana alipigwa risasi na kufariki pale pale, wenzake wazoefu walitoroka. Wazazi wake walisikitika sana kumkosa mtoto wao. Lakini wana jamii walisikika wakisema ama kweli sikio la kufa halisikii. Endapo angewasikiliza wazazi na wote waliomkanya tangu utoto wake, haya yote yasingemkuta. Kwa upande wa jamii na taifa, nguvu kazi ilipotea kwenye nyanja za kielimu, kiuchumi na kisiasa. Kisa hiki kina funzo kubwa kwa vijana wetu. Yawapasa wawe wasikivu, wazingatie yale wanayoaswa na wakubwa zao kwani “asiyesikia la mkuu huvunjika guu”.The Healing Hands Project

We are excited to launch the #HealingHands project. The project supports interpersonal counseling, group talk therapy and psychoeducation resources to be delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. It also promotes the economic growth of grandmothers who are trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program #mhGAP. Income generated from sales of the jewelry will also support the sustainable implementation of accessible psychosocial interventions among underserved communities. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay posted.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #ArtTherapy

Kushinda na Kushindwa ni Sehemu ya Maisha ya Binadamu

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi …

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Katika maisha watu huwa na shauku/hamu ya kutaka kufikia malengo fulani. Inategemea sana na aina na kiwango cha shauku alicho nacho mwanadamu. Ukubwa/udogo wa shauku aliyonayo mwanadamu ndio msingi wa kushinda au kushindwa. Shauku kubwa huleta ushindi mkubwa. Hali kadhalika, kama hakuna shauku na ari ndani ya nafsi ya mtu siyo rahisi kupata ushindi. Ari, shauku na nia thabiti ni vitu muhimu sana vinavyohitajika kufikia malengo/ushindi ambao ni kiu ya kila mwanadamu.The Healing Hands Project

We are excited to launch the #HealingHands project. The project supports interpersonal counseling, group talk therapy and psychoeducation resources to be delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. It also promotes the economic growth of grandmothers who are trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program #mhGAP. Income generated from sales of the jewelry will also support the sustainable implementation of accessible psychosocial interventions among underserved communities. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay posted.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #ArtTherapy

Kikulacho Ki Nguoni Mwako

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi …

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Mara nyingi binadamu huathiriwa na binadamu mwenzake. Matatizo tuyapatayo katika maisha huweza kusababishwa na watu tunaoishi nao kwa karibu. Ni watu ambao tunawaini sana na hata kuwashirikisha yale ya moyoni. Watu hawa huweza kutumia taarifa/siri zetu kama fimbo ya kutuchapia. Hii ina maana kuwa yatupasa kuwa waangalifu kwenye mahusiano yetu mbali mbali. Kumbuka, mara nyingi, adui yako ni yule yule anayekujua sana, aliyekuzoea sana na anayekula pamoja nawe.The Healing Hands Project

We are excited to launch the #HealingHands project. The project supports interpersonal counseling, group talk therapy and psychoeducation resources to be delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. It also promotes the economic growth of grandmothers who are trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program #mhGAP. Income generated from sales of the jewelry will also support the sustainable implementation of accessible psychosocial interventions among underserved communities. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay posted.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #ArtTherapy

Ukiinuliwa Tulizana

Masimulizi …

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Alitokea panya mmoja kwenye kijiji cha jirani. Panya huyo alimeza kipande cha dhahabu cha mwenye nyumba ya jirani. Mwenye nyumba hiyo alipogundua kuwa dhahabu yake ilikuwa imemezwa na panya aliamua kumtafuta mwindaji ili amtafute yule panya na kumwua ili aipate dhahabu yake. Kitendo hicho cha mwindaji kumtafuta panya kiliwashangaza sana wanakijiji kwa sababu panya walikuwa wengi pale kijijini kwao na walikuwa wanaishi kwenye mkusanyiko na hivyo kuwa pamoja daima. Walijiuliza, mwindaji atamtambuaje huyo panya? Lakini katika hali isiyo ya kawaida alitokea panya moja ambaye alianza tabia ya kujitenga tenga na panya wenzie. Hivyo mwindaji alipofika wala hakupata shida kabisa kwani moja kwa moja alimlenga yule panya ambaye alikuwa hachangamani na wenzie. Mwindaji na mwenye nyumba walimpasua yule panya na kweli wakakuta kile kipande cha dhahabu. Mwenye nyumba alishangaa na kufurahi sana. Hatimaye alimuuliza mwindaji kwamba alijuaje kama ni huyo panya aliyemeza ile dhahabu? Mwindaji alimjibu kiurahisi sana kwa kusema: “wapumbavu wakipata utajiri huwa hawapendi kujichanganya na wenzao. (When stupid people get rich they don’t mix with others) Somo lingine la nyongeza na la busara ni kwamba ukifanikiwa au ukibarikiwa kupata utajiri inakupasa uache majivuno ama majigambo. Ni vema ukabaki kama vile ulivyokuwa mwanzo. Utu wako utabakia kuwa wa thamani mbele za watu.The Healing Hands Project

We are excited to launch the #HealingHands project. The project supports interpersonal counseling, group talk therapy and psychoeducation resources to be delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. It also promotes the economic growth of grandmothers who are trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program #mhGAP. Income generated from sales of the jewelry will also support the sustainable implementation of accessible psychosocial interventions among underserved communities. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay posted.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #ArtTherapy

%d bloggers like this: