UNAPOFANYA KAZI NI ADHA TU, MAVUNO YAKIWA TAYARI NI VICHEKO

Grace Mshanga
Wisdom&Wellness Supervisor

Temeke & Ubungo,Dar-es-Salaam

Katika hali ya kawaida binadamu kufanya kazi ni adha lakini mapato yapatikanapo ni kicheko. Hivyo vijana na wana ndoa wapya huhamasishwa kufanya kazi kwa bidii ili kupata mavuno bora na mengi ili kujitunza wenyewe na familia zao.

KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA


Paulina Ngwawasya
Wisdom&Wellness Supervisor

Ilala & Kinondoni, Dar-es-Salaam


Mwanadamu peke yako huwezi kufanikisha malengo yako katika maisha kwa kujitenga, unahitaji ushirikiano. Pia ina maana kwamba ushirikiano katika jamii ni muhimu sana kwani ushirikiano huleta maendeleo na mafanikio mazuri katika jamii au kazi. Msemo huu unatukumbusha kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

KABLA HUJADANGANYWA NA WENZIO HUJAFA

Morris Lekule
Director of Programs & Sustainability

Ni mara nyingi unapodanganywa na mwenzio, marafiki au rika kwa kupotezana – sasa usipokuwa na akili ni rahisi kutumbukia kwenye shida. Hivyo basi kama utapokea ushauri unatakiwa kutumia na akili yako pia. 

MTEMBEZI HULA MIGUU YAKE

Suzan Njana
Wisdom&Wellness Counselor

Kigamboni, Dar-es-Salaam

Mtu mvivu mara nyingi ni mtembezi na anapenda kuishi kutegemea utembezi wake kula chakula atakachobahatika katika matembezi yake.Huyu ni mvivu,hana kazi maalumu na mtegemezi. Ndugu na jamii inayomjua humwita mtembezi hivyo hula miguu yake kwa kubahatisha chakula njiani kwa watu wanaomsaidia

Watu wa aina hii wanaweza kubadilika tabia ya uvivu na mtembezi kutokana na maonyo ya watu wanaoishi nao kwa kuwashutumu juu ya tabia hizo zinazowakosesha uhakika wa maisha.Taratibu baadhi yao hupunguza au kuacha na kuanza kushiriki kazi hadi kuwa na bidii katika zinazowaingizia kipato; hatimaye kubadilika na kuboresha hali zao za maisha.

Ushauri wa jamii inayowazunguka waathirika hawa huwa siyo rasmi.Maneno na matendo yao juu ya waathirika hutokea  kuwa fundisho kwao kwa kusikia,kuguswa,hadi kubadilika na kuwa watu wazuri.

VUNJA JUNGU HUWA ANA UWOGA, HUJIFUNGIA KUHOFU AKITOKA WATASEMA NI YEYE KAHARIBU

Paulina Ngwawasya
Wisdom&Wellness Supervisor

Ilala & Kinondoni,Dar-es-Salaam

Watu waoga huchelewa kujitokeza mbele ya watu kwa hofu kuwa watasingiziwa maovu. Hii huleta madhara makubwa katika jamii.

%d bloggers like this: