Rustica TembeleFounder & CEO Inaweza kuwa na maana ya mtu kufikishwa pabaya pale anapofanya uchaguzi uliopitiliza wa kitu chochote na hatimaye kupata kitu kisicho kizuri. Mathalani, mwanaume anayechagua sana mke au mwanamke anayechagua sana mume anaweza kuishia kupata mke/mume asiyefaa. Usemi huu unaweza kutumika kwa kuwaasa watu wanaofanya chaguzi zilizopita kiasi kwenye maisha.
Category Archives: Wisdom&Wellness Talks
KWA MUOGA HUWA HAKUNA KILIO
Morris LekuleDirector of Programs & Sustainability Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth Wale wanajifanya ni shujaa mbele ya hatari ndiyo wanaopata matatizo mfano kufa, kujeruhiwa.
MFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUA
Christina MandeWisdom&Wellness Counselor Kizinga, Dar-es-Salaam Maana yake ni kama una maradhi yanayokusumbua humwambii mtu ili upate msaada wa matibabu basi mwisho wake ni kifo. Au kama una matatizo mazito na ukaamua kukaa kimya basi unaweza kuishia na msongo wa mawazo au kifo.
DAMU NZITO KULIKO MAJI
Grace MshangaWisdom&Wellness Supervisor Temeke & Ubungo, Dar-es-Salaam Hii inawaasa familia/wanandugu kujaliana na kuthaminiana zaidi. Msemo huu unatumika kuwaasa watu wenye tabia ya kudharau/kutojali ndugu zao.
HABA NA HABA HUJAZA KIBABA
Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Pugu, Dar-es-Salaam Hii hutumika kuwahimiza watu kuweka akiba, kwani kwa kuweka kidogo kodogo hatimaye utakuwa na akiba ya kutosha Msemo huu hutumika kuwaasa watu ambao wana tabia ya kutumia kila wapatacho bila kuweka akiba angalau kidogo. Watu wa namna hii hupata matatizo huko mbeleni kwa kukosa hata mahitaji ya msingi.
NIAMBIE RAFIKI ZAKO NI NANI, NAMI NITAKUAMBIA WEWE NI NANI
watu wakijua marafiki unaofuatana nao wanaweza wakajua wewe ni mtu wa aina gani kutokana na tabia za wale rafiki zako
SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI
Suzan MwingiraAdministrative Assistant Msemo huu unatufundisha wazazi na walezi kuwalea na kuwafundisha watoto katika maadili na mienendo mizuri ya tabia. Hii huwasaidia wanapokuwa katika mazingira yanayowazunguka waweze kukubalika. Mtoto anapofundishwa angali bado mdogo inamsaidia kujua jambo zuri na baya kadri anavyoendelea kukua katika maisha yake. Hivyo itamsaidia pindi atakapokuwa mkubwa kukubalika katika jamii na hasaContinue reading “SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI”
UKIJENGA UHUSIANO NA MTU MWENYE UCHU NAWE UTAKUWA NA UCHU
Morris LekuleDirector of Programs & Sustainability Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth Ukijenga tabia na mtu mwenye tabia fulani lazima na wewe utakuwa na hiyo tabia, mfano kibaka, mwizi.
WAPIGANAPO FAHARI WAWILI ZIUMIAZO NI NYASI
Christina MandeWisdom&Wellness Counselor Kizinga, Dar-es-Salaam Katika familia, kama baba na mama wanagombana kila wakati, watoto ndio wanaoteseka kwa kukosa huduma za msingi hasa kama itatokea baba na mama wanatengana/kuachana.
KATIKA MAISHA KUNA KUPATA NA KUPOTEZA
Grace MshangaWisdom&Wellness Supervisor Temeke & Ubungo,Dar-es-Salaam Usemi huu huhamasisha kutunza utajiri. Ukipata utajiri uwe mwangalifu sana. Kwa mfano, inawezekana ulikuwa na mabasi ya abiria 10, mwisho ukapoteza kila kitu ukakosa hata baiskeli ya magurudumu mawili.