USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA

Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Mangaya, Dar-es-Salaam Usemi huu hutumika kuhimiza au kuwafunza watu kurekebisha mambo kabla hayajaharibika kabisa. Kwa mfano, nguo ikitatuka kidogo shona usiiache ichanike yote utakuja kushindwa kuirekebisha. Kwa hapa ilivyotumika ukuta ukiwa na ufa uzibe la sivyo utaanguka na kukubidi ujenge ukuta mzima.

NDEGE MOJA MKONONI NI WA THAMANI KULIKO KUMI WALIO PORINI

Rustica TembeleFounder & CEO Maana yake ni kidogo chochote ulicho nacho ni cha thamani kuliko vingi ambavyo haviko mikononi mwako.  Msemo huu unaweza kutumika kwa kuwaasa watu wenye tabia ya kudharau kidogo walichonacho na kushabikia/kutamani kikubwa wasichokuwa nacho.. 

NDEGE MJANJA HUNASA KWENYE TUNDU BOVU

Rustica TembeleFounder & CEO Inaweza kuwa na maana ya mtu kufikishwa pabaya pale anapofanya uchaguzi uliopitiliza wa kitu chochote na hatimaye kupata kitu kisicho kizuri. Mathalani, mwanaume anayechagua sana mke au mwanamke anayechagua sana mume anaweza kuishia kupata mke/mume asiyefaa. Usemi huu unaweza kutumika kwa kuwaasa watu wanaofanya chaguzi zilizopita kiasi kwenye maisha.