kitu kizuri hakiihitaji matangazo, uzuri wake huonekana kwa uwazi, lakini kitu kibaya huhitaji kutangazwa na hutembezwa ili watu wakione
Category Archives: Wisdom
MALI BILA DAFTARI HUPOTEA BILA HABARI
Suzan MwingiraAdministrative Assistant Msemo huu unamaana kwamba ni vema kuweka kumbukumbu za vitu vyako katika mahali pa usalama na katika mpangilio mzuri au kupangilia kazi zako kwa ufasaha zaidi ili kukuwezesha kujua, kutambua kwa urahisi mwenendo mzuri wa kazi zako au biashara yako.
MGAA GAA NA UPWA HALI WALI MKAVU
Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Pugu, Dar-es-Salaam Hii hutumika kuhimiza watu kufanya kazi kwani kwa kufanya hivyo hutolala njaa. Katika mfano huu, mvuvi hali chakula bila mboga.
UKIPENDA BOGA, UPENDE NA MAUA YAKE
Christina MandeWisdom&Wellness Counselor Kizinga, Dar-es-Salaam Ukimpenda mtu mpende na makandokando yake. Ina maana kuwa unapompenda mtu uwe tayari kupenda mazuri yake pamoja na yale ambayo hayakupendezi. Hali kadhalika, wapende ndugu zake na wa wale wote anaohusiana nao, usibague.
HAKUNA NJIA NDEFU ISIYO NA MWISHO
Grace MshangaWisdom&Wellness Supervisor Temeke & Ubungo,Dar-es-Salaam Hii huwafundisha na kuwaweka tayari wanandoa wapya kuwa hata tatizo liwe kubwa na limedumu kwa muda kiasi gani, mwisho wake ni kusamehana na kuishi kwa furaha na amani kama mwanzo.
UNAPOFANYA KAZI NI ADHA TU, MAVUNO YAKIWA TAYARI NI VICHEKO
Grace MshangaWisdom&Wellness Supervisor Temeke & Ubungo,Dar-es-Salaam Katika hali ya kawaida binadamu kufanya kazi ni adha lakini mapato yapatikanapo ni kicheko. Hivyo vijana na wana ndoa wapya huhamasishwa kufanya kazi kwa bidii ili kupata mavuno bora na mengi ili kujitunza wenyewe na familia zao.
KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA
Paulina NgwawasyaWisdom&Wellness Supervisor Ilala & Kinondoni, Dar-es-Salaam Mwanadamu peke yako huwezi kufanikisha malengo yako katika maisha kwa kujitenga, unahitaji ushirikiano. Pia ina maana kwamba ushirikiano katika jamii ni muhimu sana kwani ushirikiano huleta maendeleo na mafanikio mazuri katika jamii au kazi. Msemo huu unatukumbusha kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
ASIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU
Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Mangaya, Dar-es-Salaam Usemi huu hutumika kuwaasa watu wasiopenda kufuata/kusikiliza wanayoambiwa na wakubwa; kwani mwishowe hufikwa na matatizo wakajuta.
UKIMTAJA CHUI FUNGA MLANGO
Morris LekuleDirector of Programs & Sustainability Sio tu chui hii ina maana kwamba ukihisi akili yako inahisi hatari fanya jambo la kujihadhari.
KABLA HUJADANGANYWA NA WENZIO HUJAFA
Morris LekuleDirector of Programs & Sustainability Ni mara nyingi unapodanganywa na mwenzio, marafiki au rika kwa kupotezana – sasa usipokuwa na akili ni rahisi kutumbukia kwenye shida. Hivyo basi kama utapokea ushauri unatakiwa kutumia na akili yako pia.