MFA MAJI HAACHI KU TAPATAPA

Christina MandeWisdom&Wellness Counselor Kizinga, Dar-es-Salaam Msemo huu huwaasa wale wote ambao wakianguka katika mipango yao usingizia mambo mengi kama watu wanamwonea wivu, wanamloga, hawampendi n.k. Hapo anaangalia alipoangukia bila kuchunguza sababu zizotuangusha ili tuzitatue na kuanza upya.

USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA

Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Mangaya, Dar-es-Salaam Usemi huu hutumika kuhimiza au kuwafunza watu kurekebisha mambo kabla hayajaharibika kabisa. Kwa mfano, nguo ikitatuka kidogo shona usiiache ichanike yote utakuja kushindwa kuirekebisha. Kwa hapa ilivyotumika ukuta ukiwa na ufa uzibe la sivyo utaanguka na kukubidi ujenge ukuta mzima.

NDEGE MOJA MKONONI NI WA THAMANI KULIKO KUMI WALIO PORINI

Rustica TembeleFounder & CEO Maana yake ni kidogo chochote ulicho nacho ni cha thamani kuliko vingi ambavyo haviko mikononi mwako.  Msemo huu unaweza kutumika kwa kuwaasa watu wenye tabia ya kudharau kidogo walichonacho na kushabikia/kutamani kikubwa wasichokuwa nacho.. 

MTAKA NYINGI NASAHA, HUMKUTA MINGI MISIBA

Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Mangaya, Dar-es-Salaam Hii hutumika kuwaasa wale wanaopenda kufanya urafiki na kila mtu au kuwafanya kama ndugu zao hukutwa na misiba mingi kwani kila tatizo la mmoja wao litamhusu yeye pia. Msemo huu unaweza kutumika kwa watu ambao wanapenda kujionyesha ni maarufu na hivyo kutaka waonekane wanashiriki kila jambo litokealo, ukweli ni kwambaContinue reading “MTAKA NYINGI NASAHA, HUMKUTA MINGI MISIBA”