Mama Sixtha Komba (M&E Officer, TEWWY) atuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na uwanja wa majadiliano hasa kati ya vizazi.
Category Archives: Wisdom
BUSARA ZIANGUKIAZO KWENYE “T” TATU
Mama Sixtha Komba anatueleza juu ya T tatu ambazo unaweza tumia katika kuyakabili matatizo ukutananayo. Akianza na fafanuzi juu ya T tatu. T1 ni Tatizo T2 ni Tatuzi T3 ni Tokeo Mama Sixtha Komba anaendelea kufafanua hizi T tatu katika nyanja mbili, hasi na chanya kwa kutumia mfano wa mwanafunzi aliyefeli mitihani yake na jinsiContinue reading “BUSARA ZIANGUKIAZO KWENYE “T” TATU”
MOYO WA MTU NI KICHAKA
Magreth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Moyo huficha siri nyingi, nzuri na mbaya. Ni vigumu kwa mtu kuelewa undani wa mtu mwingine.
USIIGE KUNYA KWA TEMBO UTAPASUKA MSAMBA
Magreth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Msemo huu ni onyo kwa wanaopenda kuiga bila kufikiri.
UZURI WA MKAKASI NDANI NI KIPANDE CHA MTI
Magreth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Usiwe mwepesi kudanganywa na unachokiona nje, ndani kinaweza kisiwe kizuri. Ni vema kuchukua muda na kukichunguza kwa kina ili kujiridhisha.
MTU MWENYE AIBU HUFIA UPENUNI MWA NYUMBA
Paulina NgwawasyaWisdom&Wellness Supervisor Ilala & Kinondoni, Dar-es-Salaam Ni vema kushirikisha watu matatizo yanayokusibu ili upate msaada na usifikie pabaya.
USITUKANE WAKUNGA NA UZAZI UNGALIPO
Margareth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Hutumika kama onyo kwa mtu anae dharau huduma muhimu anayopewa, kwani siku nyingine ataihitaji tena. Usemi huu unaweza kufananishwa na ule usemao “Baniani mbaya kiatu chake dawa.”
WAKATI UKUTA
Caroline SwaiWisdom&Wellness Supervisor Kigamboni,Kinondoni & Ubungo,Dar-es-Salaam Inatufundisha kuwa kila jambo linatakiwa kufanyika kwa wakati wake kama lilivyopangwa. Vinginevyo ukichelewa, utakosa mengi, unaweza pata hasara na itakuwa haina maana kwako. Msemo huu unafanana na ule usemao “Chelewa chelewa utakuta mwana si wako”.
MMOJA SHIKA SI KUMI NENDA UJE
Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Mangaya, Dar-es-Salaam Usiache au kudharau kitu ambacho tayari unacho mkononi ukitegemea utapata vingi baadaye.
ULIMI NI PAMBO LA MDOMO
Mary KinguWisdom&Wellness Meditation Garden Tandale, Dar-es-Salaam Ulimi ni kiungo muhimu katika mazungumzo ya kila siku, unapotumiwa vibaya huleta madhara makubwa. Usemi huu unatupa fundisho la kutumia vizuri ulimi katika mazungumzo, iwe kwenye familia, jamii, na hata katika taasisi mbalimbali.