Mama Sixtha Komba (M&E Officer, TEWWY) atuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na uwanja wa majadiliano hasa kati ya vizazi.
Category Archives: Swahili Wisdom
BUSARA ZIANGUKIAZO KWENYE “T” TATU
Mama Sixtha Komba anatueleza juu ya T tatu ambazo unaweza tumia katika kuyakabili matatizo ukutananayo. Akianza na fafanuzi juu ya T tatu. T1 ni Tatizo T2 ni Tatuzi T3 ni Tokeo Mama Sixtha Komba anaendelea kufafanua hizi T tatu katika nyanja mbili, hasi na chanya kwa kutumia mfano wa mwanafunzi aliyefeli mitihani yake na jinsiContinue reading “BUSARA ZIANGUKIAZO KWENYE “T” TATU”
MOYO WA MTU NI KICHAKA
Magreth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Moyo huficha siri nyingi, nzuri na mbaya. Ni vigumu kwa mtu kuelewa undani wa mtu mwingine.
USIIGE KUNYA KWA TEMBO UTAPASUKA MSAMBA
Magreth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Msemo huu ni onyo kwa wanaopenda kuiga bila kufikiri.
UZURI WA MKAKASI NDANI NI KIPANDE CHA MTI
Magreth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Usiwe mwepesi kudanganywa na unachokiona nje, ndani kinaweza kisiwe kizuri. Ni vema kuchukua muda na kukichunguza kwa kina ili kujiridhisha.
MTU MWENYE AIBU HUFIA UPENUNI MWA NYUMBA
Paulina NgwawasyaWisdom&Wellness Supervisor Ilala & Kinondoni, Dar-es-Salaam Ni vema kushirikisha watu matatizo yanayokusibu ili upate msaada na usifikie pabaya.
USITUKANE WAKUNGA NA UZAZI UNGALIPO
Margareth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Hutumika kama onyo kwa mtu anae dharau huduma muhimu anayopewa, kwani siku nyingine ataihitaji tena. Usemi huu unaweza kufananishwa na ule usemao “Baniani mbaya kiatu chake dawa.”
WAKATI UKUTA
Caroline SwaiWisdom&Wellness Supervisor Kigamboni,Kinondoni & Ubungo,Dar-es-Salaam Inatufundisha kuwa kila jambo linatakiwa kufanyika kwa wakati wake kama lilivyopangwa. Vinginevyo ukichelewa, utakosa mengi, unaweza pata hasara na itakuwa haina maana kwako. Msemo huu unafanana na ule usemao “Chelewa chelewa utakuta mwana si wako”.
MKWE/KIJANA ALIYEOA KWENU UTAMJUA KWA MAVAZI YAKE
Grace MshangaWisdom&Wellness Supervisor Temeke & Ubungo, Dar-es-Salaam Mvulana aliyeoa katika familia yenu lazima awe nadhifu, aongee kwa heshima, awe na juhudi katika kazi – hivi ndivyo vitu vitakavyomtambulisha kuwa ni mkwe wenu anayefaa.
JITAHIDI KUWA NA MARAFIKI WAZURI WENGI LAKINI AMINI WACHACHE WANAOKUFAA
Christina MandeWisdom&Wellness Counselor Kizinga, Dar-es-Salaam Marafiki wazuri watakuunga mkono kwa mambo yote mema unayofanya au unayofikiri kufanya na pia kutokushabikia kufanya maovu. Hawatasita kukuambia ukweli pale utakapofanya au kufikiria kufanya maovu na daima watakuelekeza njia inayofaa.