Maji ya moto katika usemi huu, tunamaanisha maneno maneno hayavunji mfupa. Ni kawaida kabisa kila siku iendayo kwa Mungu sisi binadamu, muda mwingi tunautumia kwa kusemana semana na kufanyiana vurugu nyingi za hapa na pale. Hata pale inapoonekana kuwa mtu anajihangaisha bila kuchoka ili kujitafutia riziki yake, vimaneno maneno huwa ni vingi sana
Category Archives: Afya ya akili
Tuwe Tayari Kufanya Kazi Wakati Wote
Kinachofuata ni kisa cha mama na mtoto wake wa kiume. Yaliyomo ndani ya kisa hiki yanaweza yakakuumiza sana kama una roho yenye huruma na ya kibinadamu
Nyoka Na Jongoo
Hapo zamani za kale, Nyoka alikuwa ana miguu lakini macho hakuwa nayo. Jongoo naye alikuwa na macho, lakini miguu alikuwa hana
Ukomo Wa Subira Yako Ndio Mwanzo Wa Husuda
Kila jambo linalofanywa na mtu yeyote lina mahali pa kuanzia. Katika kuanza jambo kunahitajika mipango thabiti ili liweze kutekelezeka. Utekelezaji wa mipango hiyo, utahusisha binadamu wengine kwa asilimia kubwa. Kwa kawaida, kipindi hicho huwa ni cha mpito
Wazazi Wana Haki Ya Kutunzwa Na Watoto Wao
Kinachofuata ni kisa cha mama na mtoto wake wa kiume. Yaliyomo ndani ya kisa hiki yanaweza yakakuumiza sana kama una roho yenye huruma na ya kibinadamu
Acha Kuishi Kwa Wasiwasi, Hapo Ulipo Bado Una Nafasi
Maisha ni kupanda na kushuka. Chochote utakachokifanya, ni lazima utapitia changamoto za aina mbali mbali. Changamoto hizo zisikufanye uishi kwa wasiwasi na pia zisikukatishe tamaa.
Tutumie Mikakati Thabithi Katika Kuwafunza Watoto Wetu Maadili Mema
Hapo zamani kulikuwa na kaka mmoja ambaye alikuwa akiwalea dada zake wawili. Aliwapenda sana na akawa karibu nao. Aliwalea vizuri na kuwapatia mahitaji yao ya msingi
Mtoto Umleavyo Ndivyo Akuavyo
Mithali hii ni ya msingi sana, kuanzia pale mtoto anapozaliwa kwani tabia ya mtu inaweza kuwa nzuri au mbaya kutegemea na alivyolelewa na kukuzwa. Mfano, kama baba anakuwa na tabia ya kufokafoka na ukali uliopitiliza kila anaporudi nyumbani, watoto wake huishi kwa kuogopa muda wao wote. Pia wanaweza wakajenga tabia ya kuwa na hofu kila wakati wanapomuona baba yao. Woga ukiwazidi pia huwafanya watoto kuwa na tabia ya uongo na hata ya unafiki. Watoto wana akili sana. Wanaweza wakaamua kuwa vile mzazi wanavyomuona anataka wawe
Mtandao Ni Uwanja Wa Ulaghai
Baadhi ya wasichana wamekuwa wakirubuniwa na baadhi ya wanaume wanaoishi nchi za nje. Warubuni na warubuniwa, hukutana kwenye mitandao ya kijamii. Utandawazi ndio chanzo kikubwa cha kuleta yote haya. Mahusiano huanzia hapo, kwenye mitandao, juu kwa juu
Fanya Kazi Vizuri Kwenye Nafasi Yako
Kazi ndio msingi wa maisha. Binadamu sote hujishughulisha na kazi ili waweze kuishi. Katika mchakato huo wa kufanya kazi, unakutana na watu wengi ambao nyote mpo kwa ajili ya kufanya kazi na kupata riziki