KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA

Paulina NgwawasyaWisdom&Wellness Supervisor Ilala & Kinondoni, Dar-es-Salaam Mwanadamu peke yako huwezi kufanikisha malengo yako katika maisha kwa kujitenga, unahitaji ushirikiano. Pia ina maana kwamba ushirikiano katika jamii ni muhimu sana kwani ushirikiano huleta maendeleo na mafanikio mazuri katika jamii au kazi. Msemo huu unatukumbusha kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

MTEMBEZI HULA MIGUU YAKE

Suzan NjanaWisdom&Wellness Counselor Kigamboni, Dar-es-Salaam Mtu mvivu mara nyingi ni mtembezi na anapenda kuishi kutegemea utembezi wake kula chakula atakachobahatika katika matembezi yake.Huyu ni mvivu,hana kazi maalumu na mtegemezi. Ndugu na jamii inayomjua humwita mtembezi hivyo hula miguu yake kwa kubahatisha chakula njiani kwa watu wanaomsaidia Watu wa aina hii wanaweza kubadilika tabia ya uvivuContinue reading “MTEMBEZI HULA MIGUU YAKE”