NDEGE MOJA MKONONI NI WA THAMANI KULIKO KUMI WALIO PORINI

Rustica TembeleFounder & CEO Maana yake ni kidogo chochote ulicho nacho ni cha thamani kuliko vingi ambavyo haviko mikononi mwako.  Msemo huu unaweza kutumika kwa kuwaasa watu wenye tabia ya kudharau kidogo walichonacho na kushabikia/kutamani kikubwa wasichokuwa nacho.. 

MTAKA NYINGI NASAHA, HUMKUTA MINGI MISIBA

Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Mangaya, Dar-es-Salaam Hii hutumika kuwaasa wale wanaopenda kufanya urafiki na kila mtu au kuwafanya kama ndugu zao hukutwa na misiba mingi kwani kila tatizo la mmoja wao litamhusu yeye pia. Msemo huu unaweza kutumika kwa watu ambao wanapenda kujionyesha ni maarufu na hivyo kutaka waonekane wanashiriki kila jambo litokealo, ukweli ni kwambaContinue reading “MTAKA NYINGI NASAHA, HUMKUTA MINGI MISIBA”

NDEGE MJANJA HUNASA KWENYE TUNDU BOVU

Rustica TembeleFounder & CEO Inaweza kuwa na maana ya mtu kufikishwa pabaya pale anapofanya uchaguzi uliopitiliza wa kitu chochote na hatimaye kupata kitu kisicho kizuri. Mathalani, mwanaume anayechagua sana mke au mwanamke anayechagua sana mume anaweza kuishia kupata mke/mume asiyefaa. Usemi huu unaweza kutumika kwa kuwaasa watu wanaofanya chaguzi zilizopita kiasi kwenye maisha.

HABA NA HABA HUJAZA KIBABA

Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Pugu, Dar-es-Salaam Hii hutumika kuwahimiza watu kuweka akiba, kwani kwa kuweka kidogo kodogo hatimaye utakuwa na akiba ya kutosha  Msemo huu hutumika kuwaasa watu ambao wana tabia ya kutumia kila wapatacho bila kuweka akiba angalau kidogo. Watu wa namna hii hupata matatizo huko mbeleni kwa kukosa hata mahitaji ya msingi.