Heri Shetani Unayemjua, Kuliko Malaika Usiyemjua

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Tupo duniani tukizungukwa na watu mbalimbali na wenye tabia tofauti tofauti. Tunaishi kwa kutegemeana maana sisi ni wanadamu ndiyo maana utaona watu wanasaidina kwa shida na raha. Zaidi ya hapo utaona kwenye jamii zetu, kuna watu wanaishi kwa kupendana kama ndugu na kufanya vitu pamoja na kushauriana kwa kila jambo linalokuja mbele zao.

Naamini tumeshuhudia hilo Mmakonde anakuwa na urafiki na Mchaga na wakaishi kwa upendo na kwa kushibana sana.

Unakuja wakati hali hiyo inabadilika. Utakuta majaribu yanajipenyeza na kuanza kuharibu umoja wao na kuanza kugombana na kutengana, na urafiki unavujika kwa lugha chafu na wakaanza kuonana kama maadui.

Ikifikia hali hiyo kila mtu anaenda upande wake na kuanza kutafuta rafiki mwingine ambae wataendana. Zaidi ya hapo tumeshuhudia wengi wakifikia maamuzi hayo, urafiki haudumu kwasababu uliyokuwa unayategemea yanakuwa sivyo. Mwisho unaanza kujilaumu na kusema, afadhali ningebaki na rafiki yangu wa awali.

Mara nyingi yanatukuta hayo kwa kukosa ufahamu wa kutambua kuwa wote ni binadamu na hakuna aliyekamilika. Jambo jepesi ni kuombana msamaha yaishe na mahusiano yaendelee. Mwisho inapelekea kumkumbuka uliyemwona shetani kuliko huyo uliyemuona malaika kwako.   

Kutokana na msemo huo nina ushauri kuwa dunia imejaa mapito, lakini msamaha na kuachilia, utaishi kwa amani ndani ya jamii. Mahusiano na watu wengine yatakuwa mazuri na uhakika wa kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo, hayatakuwa magumu kwako.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: