Thamani Ya Mbwa Huisha Mwisho Wa Mawindo

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Ni ukweli usiopingika kuwa katika maisha thamani ya mtu huisha pale anapokuwa hayuko tayari tena ama hana uwezo wa kuendelea kutoa msaada. Hii inaweza kutokea kutokana na hali yake kiuchumi kupungua au kutetereka.

Katika kipindi hicho hata kama ulikuwa mtoaji kila mtu uliyemsaidia anaweza kuwa mbali na wewe, ataanza kujitenga. Kama ni mtu asiye na imani, mathalani, kuwa na Mungu, mtu anayepitia mikasa kama hiyo, hii anaweza kuchanganyikiwa na kufa mapema kwa usongo wa mawazo na magonjwa mengine sambamba na hayo. 

Dunia hii ni ya ajabu, pia ni kitu dhaifu sana, lakini usicheze nacho. Dunia inaweza ikakudanganya na hata kukutoa kwenye msitari. Wakati huo hata thamani yako inaweza isiwepo tena.

Sambamba na usemi huu kuna ule unaosema, “Mkono mtupu haulambwi”. Kwa mwindaji, mbwa huwa ni wa muhimu sana anapoenda kuwinda. Mara amalizapo na kupata mawindo yake, mbwa anakuwa hana thamani tena kwake. Inaweza ikatokea pia, endapo mbwa huyo atamsogelea binadamu huyo, anaweza hata akampiga na kumfukuza ili akakae mbali naye. 

Hii ni tabia ni ya ajabu kwa binadamu. Wakati wanaelekea kuwinda mbwa huyo alikuwa wa muhimu sana kwake. Alikuwa akimbembeleza na kumfanya kama rafiki yake wa kweli.

Binadamu ndivyo tulivyo kwenye hii dunia, mara nyingi tunampenda mtu wakati tuna uhitaji naye. Tatizo likiisha huwa hatumkumbuki yule aliyetufikisha hapo na mara nyingi huwa hatuna haja nae tena. 

Pamoja na uzuri wake, dunia hii ni chombo dhaifu sana, chombo chenye vurugu nyingi na za kutosha. Tusipokuwa waangalifu, tunaweza tukajikuta mahali pabaya. Yatupasa kuchukua tahadhari ili tuweze kuendana nayo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: