Maisha Mashenzi

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Maisha ni zawadi ambayo Mungu ametupa wanadamu ili tuishi kwa mafanikio kadiri alivyotuahidi maana vyote chini ya jua ni vyetu kwa hiyo kila mtu awe na maisha mazuri na yenye baraka.

Katika maisha yetu ya kila siku toka tuzaliwe hadi leo, tumeshuhudia mambo mengi kutoka kwa marafiki zetu, majirani zetu, wafanyakazi wenzetu na hata kutoka kwa ndugu zetu wa kwenye koo zetu, jinsi watu wanavyoendesha maisha yao. 

Msemo wa maisha ni mshenzi, umenigusa sana. Ukichunguza kwa undani, utaona watu wengi wapo kwenye kasi ya ajabu ya kushindana nani ni zaidi ya mwenzie. Tukiwa kwenye nani zaidi ya mwingine, ndipo tunaona kuwa yule aliyetupa vyote, mwenye mamlaka na maisha yetu yote, tunamsahau. Huyu si mwingine bali ni Mungu ambaye ni Muumba wetu. Mara nyingi, tunajikuta tunaingia kwenye kutafuta mbinu nyingine za mkato ambazo zinaweza kukubeba juu kwa juu mpaka ukajiona wewe ni zaidi hakuna mwingine zaidi yako. Hali hii tumeishuhudia mara nyingi. Mathalani, fulani alikuwa na pesa nyingi, kwa maana ya kuwa alikuwa tajiri sana. Mwisho wake anakuwa masikini kupindukia. Hivyo, inabakia kuwa ni historia iliyobeba maumivu yenye fedheha kubwa. 

Maoni yangu ni kwamba tujitahidi kutafuta maisha mazuri yenye mafanikio kwa njia iliyo halali. Tukifanya hivyo, maisha yetu yatakuwa na baraka kutoka kwa Muumba wetu. Maisha mashenzi ni yale maisha ambayo unayaishi kinyume na mapenzi ya Mungu. Mwsho wake, unaishia kupata aibu na fedheha ambayo inaweza kudumu mpaka kwenye uzao wako.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: