Akufaaye Kwa Dhiki Ndiye Rafiki

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kulikuwa na bawana mmoja ambaye alitaka kujua rafiki yake wa kweli ni nani. Siku moja alimwambia mkewe, “Mke wangu andaa chakula kizuri na kingi. Nataka kula na rafiki zangu wapenzi”. Mkewe alifanya kama alivyoamriwa na mumewe. Akanunua kila aina ya mapochopocho na kupika. Pia alinunua vinywaji vingi vya kutosha kwa ajili ya wageni wake.

Baada ya kumaliza kutayarisha kila kitu, alimwagiza mkewe aandae na kuweka mezani tayari, ili wageni wakifika waweze kukuta kila kitu kiko tayari. Hatimaye yule bwana akamwambia mkewe afunge mlango wakati yeye anaenda kuwaita wageni. Akatoka nje huku akipiga kelele ya kuomba msaada kuwa nyumba yake ilikuwa inaungua moto kule ndani.

Majirani wengi walibaki ndani kwao ila wapita njia na baadhi ya majirani wachache walikimbilia ndani kutoa msaada kutokanana na kilio chake. Yule bwana alifungua mlango watu wakaingia naye. Walipofika ndani walishangaa kuona kuwa hakukuwa na moto wowote, bali walikuta chakula mezani. Jambo la kufurahisha zaidi, walikaribishwa mezani ili waweze kushiriki karamu ile. Watu walikula na kusaza, wakamshukuru mwenyeji wao kabla ya kuondoka na kuelekea makwao.

Mkewe alimuuliza mume wake maana ya tukio hilo. Swali hili lilikuja baada ya mke wake kutowaona hao marafiki ambao alikuwa anawategemea na aliokuwa amewaandalia hicho chakula. Yeye alitegemea kuwaona hao wageni na majirani zake ambao walikuwa na mahusiano ya kiujirani. Badala yake walikuja watu ambao hakuwategemea kabisa maana walikuwa wengine mafundi wa gereji, wabeba mizigo na wapita njia tu. Mke kwa mshangao alimuuliza mume wake, “Hao ndiyo rafiki zako”?

Yule bwana akamjibu mke wake, “Ndiyo mke wangu hawa ndiyo rafiki zangu maana walinikimbilia kunipa msaada wa kuniokoa nilipolalamika kwamba nyumba yangu ilikuwa inaungua moto. Watu hawa bila kujali, waliacha shughuli zao wakaja haraka. Naamini ningesema kuna sherehe wangekuja wale ambao ulikuwa unawatarajia. Lakini nilisema ninaomba msaada waniokoe, ndiyo hawa wamekuja. Hawa ndiyo rafiki zangu wa ukweli”. Wahenga walinena, ‘Akufaaye kwa dhiki, ndiye rafiki’.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: