Usiogope Kuchukiwa, Ogopa Kulaumiwa

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Chuki na lawama ni mambo ambayo yanakuja kwa kasi sana katika maisha ya jamii zetu. Mbaya zaidi, katika mahali pa kazi, hayo yameanza kuwa ndio maisha ya wengi. Kwenye sehemu ya kazi, chuki huja kuhusiana na utendaji wa kazi wa mtu. Kuna ambaye anachukiwa tu kwa sababu ya utendaji wake wa kazi na umakini katika kuitenda kazi aliyokabidhiwa na mkuu wake wa kazi.

Hapo sasa, kwa wale wavivu ambao hawapendi kujituma, lazima watachukia na kulaumu na kumsema vibaya yule anayejituma, Uvivu wao unakuwa ni adhabu kwa wengine. Mtu anayejituma, mara nyingi hupewa majina mengi ya kejeli, kama vile anajipendekeza, anajifanya yeye ni bora kuliko wao na maneno mengi tu ya kuudhi na kuumiza.

Katika hali ya kawaida, mtu wa aina hiyo, mwenye kujituma, ni dhahiri kuwa lazima atapendwa na msimamizi wake wa kazi. Kuna sababu nyingi tu za kumpenda mtu kama huyu. Moja ya sababu kubwa ni kwamba, mtu wa namna hii huokoa muda kwa kufanya kazi kwa bidii na pia huongeza uzalishaji wa kampuni ama shirika analofanyia kazi. Hapo lawama ndio huwa zinazidi.

Ni kawaida katika jamii zetu mtu kuchukiwa pale mtu anapofanikiwa katika maisha yake. Mara nyingi watu wa namna hii huwa hata hawajui walianzia wapi na jinsi walivyopata mafankio yao kwani wao walikuwa wanatekeleza tu wajibu wao. Ikumbukwe kuwa maisha yana pakuanzia, ni sawa na kupanda ngazi, huwezi kufika ngazi ya tatu bila kupitia ya pili. Maisha ndivyo yalivyo.

Usemi huu unatufundisha kuwa ukiogopa kuchukiwa, basi subiria kusemwa vibaya au kuharibikiwa . Acha wakulaumu ili mradi mambo yako yanaenda vizuri. Mwisho wa siku chuki zao zitafikia mwisho.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: