Adui Hatoki Mbali

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Usemi huu unatufundisha jinsi tunavyopaswa kuishi na jamii na marafiki wanaotuzunguka. Ni vizuri kuwa karibu na hao watu kwa sababu hata maandiko yamesema binadamu tupendane na tusaidiane. Tunapaswa kujua kuwa hayo yote tunatakiwa tuyafanye kwa kiasi na kwa makini sana. Kumbuka, wema wako unaweza kukupeleka kwenye kilio. Sio kilio cha kufiwa, bali tunaongelea kilio kitokanacho na matatizo utakayoyapata baada ya hapo. 

Wahenga walisema, ‘Kikulacho ki Nguoni Mwako’. Mara nyingi marafiki ndio huwa wanakuja kuwa maadui wa kutisha. Hii ni kutokana na sababu ya kwamba, rafiki yako ndiye aliye karibu yako na ndiye anayekujua vizuri. Yeye ndiye ajuaye siri zako au mambo yako yaliyo mengi. Kwa maana hiyo kwake yeye, kukusaliti inakuwa ni kitu rahisi sana, kwa njia moja au nyingine.

Tuwe makini sana na marafiki. Tusiyaanike mambo yetu yote kwao. Ikumbukwe kwamba binadamu wengi huwa hawapendi wenzao wapate au wawe na hali vizuri zaidi kuwashinda wao. Mara nyingi sana, uadui huanzia hapo. Unaweza kushangaa pale unapomkuta mtu anakununia au kukukasirikia tu bila sababu yoyote. Hata ukitafakari sababu za kununiwa ama kukasirikiwa, hupati jawabu. Kama ni wema, tenda tu bila kusubiri shukurani. Wahenga pia walinena, ni heri ukutane na mnyama mkali kuliko binadamu mnafiki. Kwa kusema kweli kabisa, mwanadamu aliye mnafiki, huchosha sana na hukosesha raha na amani kwenye jamii.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: