Njia Ya Mkato Tamu, Lakini Ina Madhara

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Mara nyingi kama mtu anataka afike haraka, anatafuta njia ya kukatisha, njia ya haraka. Njia hiyo inaweza kuwa nzuri pale tu utakapofanikiwa kufika kule uendako. Kuna wakati lakini njia ya mkato inaweza ikakupoteza na ukashindwa kufika uendako. Kuna baadhi ya binadamu, hupenda kutafuta mafanikio kwa kupitia njia ya udanganyifu, kama kutapeli wenzao. 

Kulikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa mtanashati sana na alionekana ana uwezo kuzidi wenzake pale mtaani. Alikuwa anaheshimika sana na watu. Pia alionekana kuwa mtu wa maana sana kwani alikuwa na fedha za kutosha. Kwa kweli alionekana kuwa mtanashati sana lakini hakukuwa na mtu aliyekuwa akijua kazi aliyokuwa akifanya na mahali alipokuwa anafanyia hiyo kazi. Kumbe yule kijana alikuwa ni tapeli na mwizi mzoefu.

Waswahili husema, siku za mwizi ni arobaini. Mtu hawezi kuendelea kufanya maovu yake milele bila kuja kuumbuka siku moja. Zilipofika arobaini zake, kijana alikamatwa akiwa anafanya uhalifu kwenye nyumba ya jirani yake. Watu wote wa mtaa mzima walikusanyika. Hawakuamini walichokuwa wako kuona. Walibakia wanamshangaa yule kijana kwani hawakutegemea kabisa kuwa alikuwa kwenye kundi hilo la wezi. Lakini hawakuishia kumshangaa tu, bali walimtembezea kipigo cha mbwa mwizi. Kijana alipoteza maisha kimzaha mzaha tu. Huo ndio ukawa mwisho wa uhai wake, mwisho wa uhalifu wake. Maisha bwana, kila mtu huvuna alichopanda.

Simulizi hii inatufundisha kuwa waadilifu wa mambo tunayoyafanya. Tamaa ya kupenda utajiri ama anasa za bila jasho zina madhara makubwa huko mbeleni. Njia ya mkato ya kujipatia utajiri usio wa halali haijawahi kumsitiri mtu na kumwacha salama. Mwisho wake huwa ni mbaya, pamoja na kifo, kama tulivyoona kwenye simulizi hii. Mazoea ya kukwapua vitu vya watu yameishia ukingoni. Inasikitisha sana. 

Tunashauriwa kutopenda vitu vya mserereko, vitu vya bure. Yatupasa tufanye kazi ili tuweze kupata mafanikio ya halali. Vitabu vya dini vinatuambia kuwa, Mungu hamtupi kiumbe wake. Ipo siku wewe usumbukaye na adha za dunia hii, utafanikiwa. Zingatia maadili yanayotakiwa kufuatwa na mwanadamu. Maisha ni mzunguko, kuna kupata na kukosa. Huwezi ukapata kila siku na hali kadhalika, huwezi ukakosa kila siku. Tumeumbwa ili tupambane na maisha na siyo tubweteke tu huku tukingojea kupata vya bila jasho. Hiyo haiwezekani kabisa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: