Tuwe Wastaarabu Na Busara Katika Maongezi

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Binadamu tunatakiwa kuishi kwa kufuata taratibu fulani zilizopo kwenye jamii, hii ni pamoja na jinsi tunavyozungumza na wenzetu. Kwa maana hiyo, ukiwa mstaarabu na mwenye busara huwezi kuuliza uliza watu maswali ambayo hayastahili kuulizwa, maswali kama: ‘Bado hujaolewa tu?….Una watoto wangapi?…Utazaa lini?…Mbona umri umeenda?…na mengine mengi.

Duniani watu wanapitia mambo mengi magumu ambayo huna taarifa nayo, wala hujawahi kuyasikia, na pengine hutakiwi kuwa umeyasikia kwani hayakuhusu. Kama binadamu, unatakiwa kuwa mwenye utu unapozungumza na wengine. Chagua maneno ya kusema. Ikiwa wewe umefanikiwa kupata vyote, epuka kuropoka maneno yasiyo na utu ndani yake kwa wenzio, maneno yanayochoma moyo, maneno ya ‘shombo’ achana nayo kabisa.

Kuna watu wanapitia changamoto za aina mbali mbali, kama vile mahusiano, uzazi, uchumi na mambo mengine ya kifamilia. Wakati unaongea na watu wowote wale, yakupasa uwe makini, chekecha na kuchambua maneno ya kuongea. Yakupasa uchague maneno ya kusema ama maswali ya kuuliza, siyo kujiropokea ovyo tu. Kila unapoongea na mtu, fikiri kwanza na ujiulize, je ingekuwa wewe unaambiwa hivyo, ungejisikiaje? Tusipende kuwaambia watu maneno ama maswali ambayo tusingependa yaelekezwe kwetu. Sote tu binadamu, tuna hisia tofauti.

Ndio maana watu wengine wanajitenga na jamii, sio kwa sababu hawana upendo na watu, laa hasha! Moja ya sababu kubwa ni kukwepa kero na mazingira ya kuongezewa stress kwenye maisha yao, ambayo tayari yanawahangaisha. Kuna watu hata sherehe na mikusanyiko ya watu wengi wanakwepa kushiriki kwa sababu tu ya kutaka kujiepusha na maswali kama hayo hapo juu.

Busara ni kuwa makini unapozungumza na watu, usiwe na maswali ya kuwakwaza wengine, au maneno yenye masimango. Maisha sio mashindano jamani. Tupendane na tushirikiane, safari yetu ni fupi sana hapa duniani.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: