Usimkumbushe Mtu Mema Yako, Acha Dunia Imkumbushe

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kusaidiana katika maisha yetu ni jambo la kawaida. Hapa duniani tunategemeana. Hakuna aliyekamilika. 

Pamoja na hivyo, kuna jambo huwa tunalifanya ambalo sio sahihi. Kuna wakati ambapo watu huanza kusemana kuhusu misaada wanayopeana. Mara nyingi, hali ya kusemana hutokea pale watu wanapokuwa wamekosana. Aliyetoa msaada mara nyingi, huanza kutoa maneno ya kashfa kwa yule aliyesaidiwa. Huwa ni matangazo, kila mtu atamwambia na kutoa maneno yasiyofaa, kama vile, “yule mnayemuona, bila mimi asingefika hapo alipofika, yaani mimi ndiye niliyemuinua”.

Tabia hii kwa kweli, siyo sahihi hata kidogo. Wewe ulitoa kwa hiari yako, tena mkiwa wawili na kwa maelewano yenu. Sasa iweje ufanye tangazo? Endapo unaona kuwa uliyemsaidia hakurudishii fadhila, wewe mwache. Fadhila unayostahili, atakurudishia Mungu. lakini maneno ya masimango siyo mazuri. 

Yule uliyemsaidia atakuja kukumbushwa siku moja na aliyemuumba kwani wema hauozi. Wahenga walisema, ‘Apandacho mtu ndicho atakachovuna’ na pia msemo mwingine unasema, ‘Ubaya haulipwi kwa ubaya’ unaweza ukatumika katika mazingira haya. 

Mwisho tunapenda kushauri kuwa tusiwakumbushe watu wema tuliowatendea, dunia ni mwalimu mzuri sana, itawakumbusha.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: