Kama Huwezi Kuwa Wa Msaada, Basi Usiwe Kizuizi

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Watu wengi wamekuwa wakilalamika kila kukicha kuwa, maisha yanazidi kuwa magumu. Hali hiyo, imemlazimisha kila mtu kupambana kwa bidii ili mwisho wa siku aweze kupata kile alichodhamiria kupata.

Katika hali halisi, ukiwa mtu wa msaada na kuwajenga watu ili waweze kufika pale wanakotaka kwenda, ni dhahiri kuwa watakukumbuka kwa msaada wako na utakuwa mfano mzuri wa rejea katika maisha yao.

Wakati huo huo, kuna baadhi ya watu huona fahari kuweka au kuwa kikwazo kwa wenzao, ambapo huwazuia wasifike kule wanakotaka kufika. Aina hii ya watu siyo nzuri kwani hukumbukwa daima kwa madhara au vikwazo walivyoweka au kusababisha katika kuchelewesha maisha ya wenzao kwenda mbele. 

Simulizi hii inatukumbusha na kutusisitizia kuwa hapa duniani tunapita tu, iko siku tutaondoka, hivyo tunapaswa kuishi vizuri kwa kusaidiana na kushirikiana na wenzetu wanaohitaji msaada. 

Pale tutakapoondoka hapa tulipo, tuwe tumeacha kumbukumbu nzuri kwa wale tulioishi nao. Tusiwawekee wenzetu vikwazo vya maisha kwa makusudi. Roho mbaya haina nafasi kwenye hii safari yetu fupi ya hapa duniani. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: