Kuvunjika Kwa Koleo Sio Mwisho Wa Uhunzi

Joyce Msai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Joyce Msai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Uhunzi ni kazi ya kufua vyuma na koleo ni kifaa kinachotumika kuchotea makaa kwenye tanuru

Kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kusimamia shughuli na kuleta mafanikio makubwa katika jamii zao. Watu hawa huwa ni muhimili wa shughuli au kazi za mahali hapo. lnawezekana mtu mwenye kuzisimamia shughuli asiendelee kuwepo mahali pale kutokana na sababu mbalimbali, mathalani, magojwa, uhamisho na sababu zinginezo zikiwa ni pamoja na kifo. 

Endapo itatokea hivyo, shughuli na kazi zilizoanzishwa zisidharauliwe na wala hazitakiwi kusimama. Shughuli hizo zinatakiwa ziendelee, zisionekane kama ndio zimefikia ukomo ama mwisho wake. Kama italazimika kuzisitisha kutokana na sababu ya mwanzilishi ama msimamizi kuondoka, hiyo haitakuwa sahihi hata kidogo. Itabidi kutafuta njia mbadala.

Katika maisha changamoto haziwezi kukwepeka, ni bora kuzitatua ili kuweza kusonga mbele. Kwa mfano, katika kampuni au familia fulani, mtu muhimu akiondoka, haimaanishi kuwa shughuli zote zitakwama ama zitakuwa zimefikia mwisho. Itakapotokea hivyo, itakuwa ni vema na busara, kutafuta namna ama njia nyingine ili shughuli na majukumu yaliyoachwa, yaweze kuendelea kama ilivyokuwa. 

Hivyo basi yatupasa tuwatumie watu wenye vipaji na upeo mkubwa ili kuzienzi na kuziendeleza shughuli na kazi zilizoanzishwa na aliyeondoka ama kutangulia mbele za haki. Hii ndo maana ya msemo huu wa ‘Kuvunjika kwa koleo, siyo mwisho wa uhunzi’. Maisha lazima yaendelea, na vivyo hivyo, shughulii lazima ziendelee kama kawaida.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: