Maisha Yameficha Matukio/Mambo Usiyotarajia

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Usemi huu unatufundisha namna tunavyotakiwa kuishi hapa duniani, siku hadi siku. Mambo ya jana sio ya leo, maana Mwenyezi Mungu ameiumba kila siku na habari zake mpya. Tupo hapa duniani na tunatakiwa kuishi kwa kutegemeana. Aliyekusaidia jana sio atakayekusaidia leo. Kila leo ina mambo yake tofauti. 

Yatupasa tuwe waangalifu na maneno tunayoongea mbele za watu. Cha msingi, wewe cheka na watu. Kamwe usiruhusu mafanikio yako yakawa dharau kwa wengine, kwani nawe hujui kesho yako itakuwaje na wala hujui kesho ta wenzio itakuwaje. 

Inawezekana unayemdharau leo ndio akawa wa msaada kwako kesho. Heshimu kila mtu jinsi alivyo, katika nafasi yake, awe masikini au tajiri. Huwezi kujua Mungu ameficha/ameweka nini ndani ya mtu huyo. Pengine kuna mambo makubwa yamejificha ndani ya yule unayemchukia au usiyempenda. Huwezi kujua siri zake Mola. 

Asiyekufaa leo, anaweza akakufaa kesho, huwezi jua. Anaweza akaja kuwa bosi wako kesho, ukabaki unashangaa. Hata yule ambaye humpendi, usimuonyeshe hivyo na wala usimchukie. 

Ni muhimu kuishi vizuri na watu. Kumbuka, kila kiumbe aliyepo hapa duniani ana makusudi/hazina kubwa ndani yake. Maisha ni mchakato, usiruhusu mafanikio yako yakawa chanzo cha dharau kwa watu. Daima kumbuka kuwa safari yetu ni fupi sana hapa duniani. Tuishi kwa tahadhari.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: