Aliyekula Vizuri Utamjua Wakati Wa Kunawa Mikono

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kama vile ambavyo binadamu hatufanani, ndivyo ilivyo katika maisha ya mwanadamu. Kuna watu ambao Mungu amewajalia kuishi maisha ya raha na ya kuridhisha. Lakini kuna wale ambao wanaishi kwa kutokuwa na uhakika wa maisha yao. Watu hawa hawaelewi pale wanapoamka, siku yao itapitaje. Vyovyote itakavyokuwa, kwao ni kwa kudra na neema zake Mungu. 

Ukichunguza vizuri, katika makundi hayo mawili kundi la kwanza ni wale ambao wana uwezo. Watu hao unaweza kuwatambua kutokana na matumizi yao na namna wanavyoishi. Wao huyaona maisha kuwa ni mepesi sana. Kwa ujumla, wao wanafurahia maisha yao bila wasiwasi. 

Kwa kundi la pili maisha yao huwa ni tofauti sana na kundi la kwanza. Maisha ya kundi la pili huwa ni yale ya wasiwasi. Mara nyingi huwa hawana uhakika na jinsi siku yao itakavyokuwa. Kwao kupitisha siku bila kuwa na chochote huwa ni kawaida kabisa. Hayo ndio maisha yao ya kawaida. Kiuhalisia, kundi hili la pili lina asilimia kubwa sana ya watu kuliko kundi la kwanza, kundi la waliobarikiwa, kundi la walio nacho.

Tofauti zilizopo katika maisha ni za kawaida kabisa. Tungekuwa sote tunafanana hapa duniani, maisha yangekuwa hayaleti shauku ya kuyaishi. Tofauti zilizopo zinaweza kuwa ni kichocheo kwa wasio nacho kujitahidi kufanya kazi kwa bidii ili nao waweze kuwa kama ‘wale’ wenye nacho. Katika maisha, kuna kupanda na kushuka, hivyo inaweza kuja siku moja na wale wa kundi la pili wakafanikiwa kuwa nacho na wale wa kundi la kwanza wakajikuta wako kundi la pili. Maisha ndivyo yalivyo, ni mzunguko. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: