Utamu Wa Muwa Kifundo

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Miwa ni zao linalozalishwa kwa wingi ili kupata sukari. Viwanda mbalimbali nchini hufanya mchakato wa kupata miwa ili kutengeneza sukari. Mtu akitaka kula muwa ni lazima amenye maganda ili aweze kutafuna hiyo sehemu nyeupe ya ndani. Majimaji yenye utamu humezwa lakini makapi hutemwa. 

Kifundo ni sehemu inayounganisha pingili za muwa. Mimi ni mlaji mzuri wa miwa. Inaposemwa utamu wa muwa ni kifundo, napingana na usemi huo, kwa sababu, kwanza kifundo ni sehemu iliyo ngumu sana. Pili, majimaji yenye utamu utamu wake ni hafifu na tatu ni sehemu isiyo na majimaji mengi kama sehemu nyeupe ya muwa.

Katika maisha unaweza kuambiwa kuwa mtu fulani ni mbaya sana hivyo ukae naye mbali. Lakini inaweza ikatokea siku moja mtu huyo unayeambiwa kuwa ni mbaya akaja kuwa jirani yako kwani amepata kiwanja karibu na wewe na hivyo kajenga nyumba sehemu hiyo karibu yako. 

Baada ya kukaa naye kwa muda unakuja kugundua kuwa mtu huyo ni mkarimu na tena ni mcheshi. Watu husema, “Ni mtu wa watu”. Anaonekana kuwa hana makuu na pia ni mtu anayejielewa sana. Kwako wewe unamuona kuwa ni jirani wa baraka sana ambaye mnaweza mkaishi kwa maelewano.

 Mara nyingi, binadamu tuna tabia ya kupenda kusikia na kuamini tunayoambiwa bila kufanya uchunguzi wa kina. Tunashauriwa kuwa tusipende kuamini kila tunachoambiwa, tutapotea. Hali kadhalika, tutakuwa hatutendi haki kwa kufanya hivyo. 

Tuache kufanya maamuzi kutokana na maneno tunayoyasikia. Tusipende kupotoshwa na watu ambao hawana uhakika na yale wasemayo kuhusu maisha ya wengine. Ni lazima tujiridhishe kwanza kabla hatujaamini ama kuchukua hatua. Unaweza kuishia pabaya. Kumbuka, binadamu ni kiumbe mzito. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: