Kuzaa Si Kazi, Kazi Kulea

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kila mtu anaweza kuzaa hata kama ana kasoro za aina yoyote. Kwa mfano, hata kichaa anayeokota makopo au matakata jalalani na kula, naye huwa anazaa. Ndivyo Mungu alivyotuumba. Kuzaa ni haki ya kila binadamu.

Inapokuja kwenye kulea, hilo linakuwa suala lingine. Kulea ni tendo la kumtunza mtoto tangu ile siku ya kwanza ya kuzaliwa hadi anapokuwa mtu mzima. Katika hali ya kawaida, watoto nao wakikua huwa wanachukua zamu ya kulea wazazi wao, hivyo kulea na hufanyika kwa zamu. Hapo ndipo tunaposema kulea ni kazi kubwa na siyo kuzaa.

Katika hali ya kuwalea watoto wetu tunatakiwa kuwalea katika misingi ya maadili mema. Pia yatupasa tuwapende sana watoto wetu. Lakini ni budi tuwe makini kutokuonyesha kwao kuwa tunawapenda sana, kwani hiyo inaweza kuwaharibu. Hali kadhalika, hata kama una pesa epuka kuwapa pesa nyingi kupita matumizi yao. Inatubidi tuwajengee watoto tabia ya kufanya kazi kuanzia wakiwa na umri mdogo. 

Watoto wafundishwe pia kusalimia watu. Wafundishwe lugha ya kutumia wanapokuwa na wakubwa, hali kadhalika, wanapokuwa na wadogo wenzao. Watoto wafundishwe kuwaheshimu watu wote waliowazidi umri, hata kama si baba zao au mama zao. Pia waelekezwe kuwa yawapasa kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu katika masomo yao ili waweze kuja kupata kazi nzuri. Wakipata kazi nzuri watapata mshahara mzuri na hivyo kuwa na maisha mazuri pamoja na familia zao. 

Daima kumbuka kuwa, hata kama mzazi una nafasi nzuri hapo nyumbani, usimuonyeshe kuwa yeye ndiye atakuwa mrithi wa mali ile wakati ukifariki. Utakapofanya hivyo utakuwa unajitengenezea bomu la kukulipua hapo wakati wowote. Akijua hilo, hataona sababu ya kujishughulisha na chohote. Zaidi ya hapo, anaweza kuwa mtu wa kijiweni ambako ataweza kujiingiza katika maisha ya kuvuta bangi na kutumia dawa za kulevya. Atakusubiri wewe mzazi ufe ili aweze kurithi. Kuna wakati anaweza akatamani ufe ama akuue kama utachelewa kufa. 

Kuna familia moja ambayo ilimlea mtoto wao kimayai mayai. Mtoto yule akiwa pale nyumbani alikuwa hasalimii watu, hafanyi kazi. Alikuwa na tabia ya kutokuaga hapo nyumbani wakati akitoka. Na akirudi alikuwa haulizwi. Akitaka pesa kutoka kwa wazazi wake, alikuwa akipewa kiasi chochote. 

Alisomeshwa kwenye xshule za kikristu. Akiwa shule alikuwa na nidhamu. Akiwa nyumbani, alijiona yuko huru. Aliendelea kuwa na tabia hiyo na hatimaye alienda Chuo Kikuu. Akiwa huko chuoni, hali ya nidhamu ilikuwa kama ya nyumbani, nidhamu iliisha kabisa. Mwishowe aliishia kupelekwa kwenye nyumba za kutunza watumiaji wa dawa za kulevya, (sorber house). 

Mama akaanza kulalamika na kusema kuwa amemkosea nini Mungu. Alilalama kuwa mwanaye alikuwa anampa kila kitu lakini leo amefikia hapo. Mwisho wake yule mama alipata msongo wa mawazo na magonjwa mbalimbali na hatimaye akafariki. 

Tunajifunza nini kutokana na simulizi hii? Ni dhahiri kuwa yule mtoto alikuwa ameharibika na malezi mabaya kutoka kwa wazazi wake. Hivyo, wazazi tunashauriwa na kuaswa kuwa tuwape malezi mema watoto wetu ili wakikua, waje kututunza na sisi wakati wa uzee wetu. Tuache tabia ya kudekeza watoto kwani sisi sote ni watu wa kupita tu hapa duniani. Safari yetu ni fupi sana.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: