Unakosa Usingizi Kwa Ajili Ya Wanaokutegemea

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Usemi huu unatulenga sisi wazazi au walezi. Mipango yetu na matumizi yanakinzana kutokana na majukumu yanayotukabili siku hadi siku. Ina maana mipango na mapato, hayo mambo mawili hayaoani. Mara nyingi, matumizi yanakuwa makubwa zaidi ukilinganisha na mapato tuliyonayo. Wengi wetu tuko katika eneo hilo. 

Hebu tuangalie mfano moja wa watu ambao wanapata mishahara. Kwa kawaida, kila mshahara wa mwezi unatakiwa kutumika kwa majukumu mengi yaliyopangwa ama yatakayojitokeza kwa mwezi huo. Inaweza kuwa watoto wamefunga shule. Wanaporudi shule wanahitaji matumizi, ada, nauli ya bus la shule, michango mbalimbali ya kidini, kanisani, ama msikitini, na michango mingine ndani ya jamii. Mwezi huo huo pia unakuwa na sikukuu mbali mbali, kama za pasaka na Eid el Fitr. Hivyo vyote vinatakiwa vitekelezwe na mshahara wa mwezi ambao mambo hayo yanatokea. 

Kusema kweli, matumizi hayo yote, yanaweza kusababisha mawazo mengi kwa mhusika, kiasi cha kuchanganyikiwa. Na ndugu nao wanakutegenea hapo hapo, kwa mshahara huo huo! Hapo kunakuwa hakuna kulala kabisa. Msongo wa mawazo utakunyemelea pasina shaka.

Hayo ni majukumu machache tu kati ya mengi. Lakini yatupasa tujipe moyo ili shughuli ziendelee kama kawaida. Ipo siku, majukumu hayo yatakuja kupita. Hayo ndio maisha ya mwanadamu, kuwajibika ndio utaratibu wetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: