Ukiona Neno, Usiposema Neno, Hupatikani Na Neno

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Neno ni umoja linaweza kuwa na silabi hata kumi lakini linatambulisha kitu mfano “keti” ni neno la silabi nne, linatambulisha kitendo fulani kifanyike. Neno na neno likiunganishwa huleta maana nzuri zaidi mfano, “Eliza, keti karibu na babu”. Hii sentensi inaeleza nani afanye nini na ni wapi.

Unaposema ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno, ina maana kubwa sana. Katika maisha yaetu ya hapa duniani, binadamu tunaishi kwa kusema maneno mengi kila uchwao. Maneno ni wingi wa neno ambayo tunayatamka kupitia ndimi zetu. Hapa masikio pia yanahusika kusikia. Ukiona neno ni tendo, umeliona likifanyika. Kwa kawaida binadamu hutenda au husema mambo aina mbili tu mazuri au mabaya.

Usemi wa hapo juu, (kichwa cha habari) unamaanisha kuwa, yule aonaye matendo mabaya au asikiaye maneno mabaya ndiye hatakiwi kusema neno ili asipatikane na neno. Endapo atadiriki kusema, kama maneno, mathalani, yalikuwa ya masengenyo, matusi , ugomvi, uzushi au uongo, itabidi ijulikane ni nani alikuwa msemaji mkuu. Hapo utakuwa umeanzisha jambo jingine. Lakini pale utakaposema mazuri hutapatikana na neno.

Kwa kumalizia, ningependa kuwakaribisha kwenye blog yetu ya TEWWY ili muweze kusoma mazungumzo ama simulizi zinazoandikwa na wanasihi, ambao ni watu wazima waliokwisha kuona mengi katika kuishi kwao. Busara za watu wazima hawa zinasaidia sana katika kutibu kwa maneno mazuri na ya hekima matatizo ambayo unaweza kuwa unayapitia katika maisha yako. Matatizo haya yanaweza kuwa ya aina mbali mbali, kama msongo wa mawazo, sonona na mengine mengi.

Usikubali kuumia peke yako kwa kubeba mzigo mzito kifuani mwako. Njoo utue mizigo, kupitia unasihi wetu, utafanikiwa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: