Upendo Unaweza Kuwa Wa Kinafiki, Chuki Huwa Ni Halisi

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Upendo ni neno ambalo huwa tunaliongelea siku zote katika maisha yetu. Mara nyingi, tunapoongelea suala hili, huwa tunakuwa na marafiki. Kwa kawaida, kuna marafiki ambao wanaweza kuwa ni wa karibu sana. Marafiki hawa huwa tuko huru nao na huweza kuelezana habari zetu hata pamoja na zile za ndani kabisa.

Mnaweza mkawa sahihi kwa kuwa wawazi kwa kiasi kikubwa hivyo, cha kuelezana kila kitu. Lakini kuna hatari pale mtakapokuja kukosana. Hapo ndipo utaelewa kama urafiki wenu ni wa kweli, ama wa kinafiki. Pale utakapoanza kuona na kusikia habari zako zote ulizomueleza zimetapakaa kila mahali na ni kwa watu ambao walikuwa hawakujui kabisa, utajua huyo/hao uliowaeleza ni watu wa aina gani. Ikumbukwe kuwa watu watakaoambiwa habari zako, wataziamini kwa vile zinasemwa au kusimuliwa na mtu ambaye ni wa karibu sana kwako. Hawatasita kuziamini habari wazisikiazo kutokana na ukaribu wenu. Watajua kuwa ni habari za kweli, hata kama ni za uongo. Tayari unakuwa umechafuliwa na mtu uliyemuona kuwa ni rafiki yako. Kumbe urafiki wenu ni wa kinafiki.

Kwa upande mwingine bora mtu awe na chuki na wewe. Mara nyingi chuki huwa ni halisi, kwani inaeleweka, na iko wazi haina kificho. Mtu akiwa na chuki nawe, huonekana wazi wazi. Mtu anayekuchukia, akikukuta unaongea na mtu, ukitoka tu, jamaa atamfuata yule uliyekuwa unaongea naye. Atampatia maneno ya chuki ili aweze kukuelewa na kukuchukulia vibaya, wakati wewe hauko hivyo. 

Wakati mwingine, binadamu anaweza kuwa kiumbe wa ajabu, aliyejaa chuki na fitna. Huweza kufanya yote haya ili aweze tu, kuifurahisha nafsi yake. 

Je lipi ni bora, kuwa na rafiki mwenye upendo wa kinafiki au kuwa na mtu mwenye chuki dhidi yako, chuki iliyo halisi? Kama binadamu, yatupasa tuwe makini. Inabidi tutafakari kwa kina. Inabidi kuangalia vema, ni mtu gani anaweza kuwa rafiki yako? Na je utakuwa na mipaka yoyote ya kumweleza mambo yako? Majibu unayo mwenyewe. Tafakari

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: