Nimekupaka Wanja Wewe Umenipaka Pilipili

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Wanja ni urembo mweusi unaopakwa na wanawake kwenye kope na nyusi kwa kwa ajili ya urembo. Pilipili ni tunda dogo linalotumika kama kiungo kwenye chakula. Pilipili ina sifa moja ya kuwasha sana. Ukiwa unakatakata pilipili, halafu ukaishika na kupeleka mkono wako machoni, adhabu utakayoipata hutakuja kuisahau. Hutaweza kulala mpaka upate dawa.

Ni kwa maana hii, mrembaji anaweza kusema, “amemremba mwenzake kwa wanja na mwenziwe kampaka pilipili”, ikiwa na maana, yeye kampaka kitu kibaya kinachowasha machoni, wakati mwenzie kamrembesha na wanja. Hayo ndiyo maisha ya wanadamu.

Hebu tuangalie simulizi hii. Katika kijiji fulani, binti mmoja aliolewa na kigogo mmoja, ambaye alikuwa tajiri na alikuwa anajulikana sana. Ndoa yao ilidumu vizuri na hata wakajaliwa kupata watoto 8. Muda ulivyozidi kwenda, kigogo huyo alipata mchepuko. Alizaa naye mtoto mmoja. Mkewe alipogundua hilo, aliamua kumchukua mtoto huyo wa mchepuko, baada ya kuachishwa kunyonya. 

Mke alipoona mume wake anazaa nje ya ndoa yake, akahisi huenda labda mume wake anataka amzalie watoto wengi zaidi. Hivyo kwake hisia hizo hazkuwa tatizo kuzitimiza. Aliendelea kuzaa watoto wengine watatu zaidi, hadi akafikisha watoto 11. 

Maskini mama huyu, kumbe wakati anaongeza namba ya watoto wake ili kumfurahisha mume wake, mumewe naye akawa anaongeza watoto wengine na michepuko yake. Aliendelea kuwazalisha michepuko wake hadi akawa na jumla ya watoto wote 15. Mke naye hakuchoka kuwachukua na kuwalea wale watoto. Alidai kuwa ni damu ya mumewe na hivyo asingependa ipotee. 

Hali kadhalika, mwanamke huyu alidai kuwa alikuwa akiwapenda watoto hao wa michepuko, sawa na watoto wake wa kuwazaa mwenyewe. Ni moyo wa utu, moyo wa uzalendo. Ni wanawake wachache wanaoweza kufanya hivyo. Kwa hakika, huyu mama alikuwa ni wa pekee.

Simulizi hii inatufundisha nini? Tunafundishwa kuwa tusilipe ubaya kwa ubaya. Mwanamke huyu kwenye kisa hiki kama angetaka kulipa kwa ubaya mambo aliyotendewa na mumewe, angeweza kufanya hivyo kiurahisi sana. 

Lakini tunaona jinsi alivyofanya, alimrudishia mume wake mema. Upande mwingine tunaona jinsi mwanaume alivyotendewa wema na mke wake. Pamoja na kupakwa wanja na mke wake, yeye alimpaka pilipili. Hii ina maana kuwa, mume alimtendea mabaya mke wake. Yatupasa tuushinde ubaya kwa wema, huo ndio ubinadamu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: