
Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).
Machozi ni yale maji yanayotoka kwenye macho. Maji hayo yanaweza kutoka Kwa ajili ya furaha ama uchungu. Kwa asilimia kubwa, huwa ni mambo ya uchungu. Machozi humwagika bila kifani pale mtu anapoondokewa na mpendwa wake. Kuondokewa na mtu, hasa yule wa karibu sana, mathalani, mtoto, mume, mke huwa ni uchungu mkubwa sana katika maisha ya mwanadamu.
Lakini kuna asilimia nyingine, machozi huwa yanawakilisha tatizo ambalo mtu alitegemea kupata majibu chanya lakini majibu yakatoka kuwa hasi. Katika hali hiyo mtu anaona akitoa machozi atafikisha ujumbe mahali panapotakiwa.
Hebu tuchukue mfano wa mtoto akiomba kitu kutoka kwa mama au baba, au kwa mtu mwingine wa karibu. Mara nyingi, jambo lake lisipotekelezwa, mtoto huishia kulia sana. Wazazi wengi huguswa na machozi hayo na hulazimika ama kujikuta ‘wakitii amri’ ya mtoto kwa sababu ya machozi hayo. Hakuna mzazi mwenye uwezo wa kuziba masikio yake pale mtoto wake anapolilia kitu fulani. Machozi ya mtoto huyo humuwezesha kupata kile anachoomba. Lakini pia, ni lazima kiwe ndani ya uwezo wa muombwaji.
Lakini pia kuna wakati mwingine, machozi huwakilisha furaha ya mtu. Pengine mmekutana na mtu ambaye muliachana muda mrefu sana. Kwa furaha, machozi yanaweza kuwatoka nyote wawili kwa sababu, inakuwa kama ndoto ama ‘muujiza’ kwa wawili nyie, kukutana wakati huo.
Kwa hiyo machozi Ni ishara ya mambo mengi mchanganyiko. Kwa sehemu kubwa yanawakilisha uchungu, lakini pia hata furaha. Machozi yanatokea kufuatana na vile mhusika alivyo kwa wakati husika. Machozi pia ni ‘tiba’ ya aina fulani kwa mwili wa mwanadamu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection