Usimtendee Mwenzako Usiyopenda Kutendewa

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Msemo huu una maana kubwa. Katika maisha, kuna kufurahi kwa aina nyingi, hasa pale watu wanapokutana, wakaongea na kutaniana. Kuna bwana mmoja alipenda sana kuwatania wenzake. Naye siku moja wenzie nao wakamtania yeye. Bila kujua, kumbe ule utani ulikuwa karibia na ukweli wa yale yanayotokea nyumbani kwake. Ulikuwa unamgusa barabara.

Hapo ugomvi mkubwa ulianza. Jamaa aliuliza kwa ukali, “Uliyajuaje hayo unayosema? Bila shaka ulikwenda kwa mke wangu wakati mimi sipo, ukayachokonoa ya nyumbani kwangu. Mambo ya kutafutana, mimi sitaki kabisa”. 

Watu waliokuwepo, wakamwambia jamaa kuwa huo ni utani tu, kama kawaida yetu. Walimhakikishia kuwa yasemwayo hayana ukweli wowote, zaidi ya utani. Walichukua muda mrefu sana kumsihi, lakini somo halikupanda kichwani mwake. Bado aliendelea kukasirika sana. Alidiriki hata kusema kuwa kuanzia siku hiyo hataki utani wa kijinga tena na mtu yeyote. Akaendelea kwa kusema, “Kama mtu atakuja kunitania, nitamkatakata na mapanga. Tusitafutane ubaya”.

Wenzake lakini walimshangaa sana maana yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kuwatania wenzake muda wote kwa maneno yasiyofaa, lakini walikuwa hawakasiriki, walijua ni utani. Walijiuliza, “Iweje yeye leo akasirike kiasi hicho”?

Hapa tunaweza kusema kuwa sisi sote tuna kitu cha kujifunza. Ni busara kutofanya yale usiyopenda kufanyiwa. Kama utani huuwezi, basi na wewe usijifanye fundi wa kutania wenzako. Yale usiyopenda kufanyiwa wewe basi na wenzio usiwafanyie. Ni lazima ujifunze na kujua kuwa, wale unaowafanyia yale usiyoyapenda wewe, ni binadamu kama wewe. Kwa nini wewe ujione kuwa uko tofauti na wale? Kwa nini wewe ujione ni wa pekee sana kuliko wale? Yatupasa, kama binadamu, tuache hizo. Sio ubinadamu hata kidogo. Wahenga pia walinena, “Mkuki kwa Nguruwe, kwa Binadamu mchungu”. Wahenga walikuwa sahihi, na kwa hali hii ya hapa, ni sahihi kuutumia na usemi huu pia.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: