Usitoe Maamuzi Wakati Una Furaha Sana

Tuko katika ulimwengu wenye vurugu na fujo zisizohesabika. Kila mtu anacho akijuacho ambacho anaona mwingine hakijui na wala hakiwezi. Ni fikira ambazo wanadamu tunatembea nazo. Furaha na huzuni ni sehemu ya maisha yetu.

Mtu Hufurahia Shida Zako, Sio Furaha Yako

Matatizo yameumbwa na kila mtu huyapata. Hakuna mtu ambaye hajawahi kupitia matatizo, na hayuko ambaye hatayapitia. Inategemea ni tatizo gani na wakati gani linakutokea.

Ishi Kadri Unavyojaliwa, Na Sio Kama Mwingine Anavyoishi

Watu wengi wana kawaida ya kupenda kujilinganisha na watu wengine. Watu kama hao hupenda kujiuliza, “kama yule yuko hivi, kwa nini na mimi nisiwe vile?”

Njia Ya Mkato Tamu, Lakini Ina Madhara

Mara nyingi kama mtu anataka afike haraka, anatafuta njia ya kukatisha, njia ya haraka. Njia hiyo inaweza kuwa nzuri pale tu utakapofanikiwa kufika kule uendako. Kuna wakati lakini njia ya mkato inaweza ikakupoteza na ukashindwa kufika uendako. Kuna baadhi ya binadamu, hupenda kutafuta mafanikio kwa kupitia njia ya udanganyifu, kama kutapeli wenzao. 

Tuwe Wastaarabu Na Busara Katika Maongezi

Binadamu tunatakiwa kuishi kwa kufuata taratibu fulani zilizopo kwenye jamii, hii ni pamoja na jinsi tunavyozungumza na wenzetu. Kwa maana hiyo, ukiwa mstaarabu na mwenye busara huwezi kuuliza uliza watu maswali ambayo hayastahili kuulizwa, maswali kama: ‘Bado hujaolewa tu?….Una watoto wangapi?…Utazaa lini?…Mbona umri umeenda?…na mengine mengi.

Hekima Ni Jambo La Msingi

Kile unachokiita baraka au ushindi kilianza kama tatizo. Mara nyingi, yule anayefanikiwa kutatua matatizo huonekana kama ana baraka au mshindi fulani hivi. Ni kawaida kwa kila mwanadamu kupata matatizo. Pale mtu anapopata matatizo, ni vema kutafuta mbinu za kupambana nayo. Wengi hujaribu kukimbia matatizo yanapotokea.

Ukishindwa Hili Leo, Kesho Utashinda Lile

Wakati sisi tunasoma shule ya msingi, ilikuwa ni madarasa manne tu, yaani la kwanza hadi la nne. Enzi hizo walizingatia sana umuhimu wa kila darasa kuwa na wanafunzi wasiozidi arobaini na tano.

Huwezi Kupanda Ngazi Ya Mafanikio Ukiwa Umeweka Mikono Mfukoni

Ni jukumu la binadamu wote kuwajibika katika maisha yetu ya kila siku. Huwezi ukafanikiwa bila kutoka jasho. Kufanya kazi kwa bidii, ndio siri kubwa ya mafanikio ya mwanadamu.