Sio Sahihi Kila Mtu Kujua Changamoto Zako

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Changamoto ni sehemu ya maisha kwa kila mwanadamu. Sote tunajua kuwa kila binadamu ana changamoto ambazo humfanya azihangaikie kutafuta ufumbuzi ama suluhisho lake.

Inawezekana jawabu lako likatoka kwa mwanadamu mwenzio. Lakini hiyo huwa ni mara chache sana kutokea. Mara nyingi, wengi wa wale wanaokupa majibu huwa ni wasambazaji wa habari zako. Hali kadhalika, watu hao wanaweza wasiwe na msaada wowote kwako. Mbaya zaidi, watu hao hao wanaweza wakatoa habari mbaya na tofauti dhidi yako, tofauti na mambo yenyewe yalivyo. 

Unatakiwa uangalie ni nani anafaa kuelezwa changamoto zako. Tua mizigo yako mahali penye usalama. Siyo kila mtu ana kifua cha kutunza ama kuhifadhi siri ama changamoto za watu. Wengine hata siri ama changamoto zao wanashindwa kuzitunza na pia kuzipatia ufumbuzi.  

Yatupasa tuwe makini katika kuanika changamoto zetu kwa watu. Wengine hufurahia na hata kusherehekea pale wanaposikia changamoto za wenzao. Kumbuka kuwa, sio kila mtu ni mwema na ni wa msaada kwako. Tafakari, fikiri vizuri kabla ya kushirikisha wengine. Binadamu ni kiumbe mzito.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: