Hakuna Tajiri Anayemjali Maskini, Na Hakuna Maskini Anayemhurumia Tajiri

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Mwenye uwezo mara zote huwa ana marafiki wengi ambao wana uwezo wa kulingana naye. Kutokana na uwezo wake, anakuwa hana muda wa kumjali maskini. Yeye huona kuwa matajiri wenzie wanaomzunguka wanamtosha kwa kila kitu. Wao ndio kila kitu kwake kwani akihitaji msaada ataupata bila matatizo.

Mara nyingi, maskini naye huwa ana chuki na tajiri. Lakini kutokana na shida alizo nazo, huwa anajitahidi kumfuata fuata tajiri hata kama atakuwa anaonyesha dalili ya kutokumkubali. Lakini kutokana na matatizo aliyokuwa nayo, hulazimishwa amfuate tajiri kwa ajili ya kutafuta msaada.

Wakati huo huo, pamoja na umaskini aliokuwa nao, bado atapenda kujiinua ili aufiche umaskini wake. Angependa kuishi kama tajiri. Hizo ni hulka za binadamu, kupenda makuu asiyokuwa nayo. Ukweli ni kwamba hata hajui tajiri alifikaje hapo alipo. Mambo yakibadilika kwa tajiri maskini yule yule anakuwa hana huruma naye. Atamcheka na kumsema bila hata kukumbuka alikotoka naye. Atasema kila maneno ya kejeli, kwamba hana kitu yule, kafilisika na kwamba hana lolote.

Lakini pia tumeona kuwa maskini wengi huishia kuwa na maisha ya kimaskini zaidi kwa kujaribu kuishi kama matajiri. Tabia ya kuiga iga siyo nzuri hata kidogo. Tunashauriwa kuwa tusipende kuishi kama ‘yule’ kwani huyo ‘yule’ unayetaka kumuiga haujui alifikaje hapo. Yakupasa uishi maisha ya kwako uliyopangiwa. Cha msingi, inakulazimu ufanye kazi kwa bidii. Ipo siku, nawe utabarikiwa kwani mgawa riziki ni huyo mmoja. Zamu yako na wewe itakuja. Kuwa na subira.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: