
Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).
Kuishi ni neno linalotokana na maisha. Maisha ni siku au miaka tunayojaliwa na Muumba wetu baada ya kuzaliwa. Wenzetu wa zamani waliishi miaka mingi sana, wengine miaka 700 mpaka 900. Nyakati hizi tulizo nazo kuishi kwingi ni miaka 100 tu tena ni kwa wachache sana. Kuishi kwingi na kuona mengi hapa anazungumziwa mtu aliyeishi miaka 50 au 60.
Kuna kisa kimoja kinachomhusu baba mmoja ambaye ameona mengi katika maisha yake. Baba huyu alizaliwa katika familia ya kawaida. Alisoma katika shule zilizojulikana kama middle schools wakati huo. Akiwa shuleni, alikutana na watoto wenziwe wenye tabia za ajabu ambazo hakutarajia kuziona kwa watoto wa ngazi ile. Alipofaulu, alikwenda sekondari. Huko alikutana na wavulana vijana wenye tabia mbali mbali, wengine wavuta bangi na wengine ni kukimbizana na wasichana tu, hata masomo hawazingatii, kwani hawana muda kabisa.
Walikuwepo wale ambao walipenda kujionyesha kuwa wao ni watoto wa matajiri, watoto wa matawi ya juu. Kulikuwepo pia na kundi waliojiita makabwela. Kundi hili lilizingatia masomo, tofauti na kundi la watoto tajiri. Baba huyu alipofika chuo kikuu, aliyaona mambo mengi yakiwa ni ya ovyo ovyo tu, ovyo kuliko yale ya shule za sekondari. Kila mtu alikuwa kivyake vyake na uhuru kibao.
Mzee huyu lakini alikazana na kile kilichokua kimempeleka pale. Alikuwa na lengo la kutimiza matamanio yake. Baada ya kumaliza digrii ya kwanza na ya pili alienda Marekani kwa ajili ya digrii ya uzamivu. Aliyoyaona huko yalikuwa ni zaidi ya yale aliyoyashangaa ya hapa nchini. Alipohitimu digri yake alirejea nchini. Aliitumia elimu yake kuwasaidia Watanzania kwenye masuala ya kuleta maendeleo.
Simulizi hii inatuonyesha kuwa uwapo na umri mkubwa unakuwa umepitia mengi, mazuri au mabaya. Kinachotakiwa ni kuonyesha msimamo wako wa maisha. Hatutakiwi kuiga mambo ya watu wengine, kwani mengine huwa siyo mazuri. Maisha ni kuchagua na kutofautisha kati ya mazuri na mabaya. Huyu mzee alifanya uchaguzi mzuri. Jambo la msingi kwetu sote, tukijaliwa kuishi miaka mingi, yatupasa kufanya uchaguzi mzuri wa maisha yetu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection