La Kuvunda Halina Ubani

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kuvunda maana yake ni kitu chochote ambacho kimekaa muda mrefu na kinatoa harufu mbaya. Na ubani ni kitu kinachotoa harufu nzuri.

Katika maisha ya ndoa kuna misukosuko mingi. Mingine inavumilika na mingine haivumiliki. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba katika kupendana kwa nyie wawili mara nyingi si nyote wawili mnakuwa mnapendana kwa dhati, yaani kupendana kwa hali na mali. 

Endapo mmoja akatokea kupenda kwa ajili ya kitu fulani, kwa mfano kwa ajili ya pesa zako wewe mwanaume au kwa ajili ya uzuri wako wewe binti, hapo ujue kuna tatizo. Hilo litakuwa siyo pendo la dhati hata kidogo. Iko siku ambapo vitu hivyo havitakuwepo. Hapo ndipo malumbano ndani ya nyumba yataanza. Hali hii inaweza ikawafikisha wawili hao hata kudaiana na hatima yao kuachana.  

Ukiangalia sababu hazitoshelezi za kuachana. Mwanamke anaweza kutaka kuachika kwa kuwa alichotegemea ni kuwa atakuwa na maisha mazuri kila siku kama vile ilivyokuwa wakati wa uchumba. Sababu kama hii haitawekwa wazi popote, itakuwa ni siri yake kuu mhusika. Mwanaume atakuwa anajitahidi kumbembeleza kwa kila namna. Lakini mwanamke atalazimisha kuondoka na kukaa kwa rafiki zake, mradi tu asiwe na huyo mwanaume. Mwanaume atajitahidi hata kwenda kwa wazazi wa binti ili mkewe arudi nyumbani. Lakini jitihada zake hazitafanikuwa, zitagonga mwamba. Na marafiki zake pia wataenda kumbembeleza mwanamke. Jitihada zote hazitafua dafu. Mwisho marafiki zake mwanaume watamsihi amsahau na kumshauri atafute mwanamke mwingine. 

Ushauri wote apewao mwanaume haumwingii kichwani. Anaukubali kinywani tu, lakini moyoni mwake kuna donda kubwa. Anafikia hatua ya kuchukua maamuzi magumu ya kujiua. Dhamira na imani yake anajiambia kuwa hatapata mwingine zaidi ya yule aliyekuwa naye, mkewe kipenzi aliyempenda kwa dhati. 

Ushauri: Kama mtu akikukataa, usiendelee kupoteza muda wako kwa kumng’ang’ania. Yakupasa usikilize ushauri wa wenzio. Fanya maamuzi, achana naye, na maisha yako hayana budi kusonga mbele. Pengine usichojua ni kwamba, mwanamke huyo tayari amekwishafanya maamuzi yake mengine. Wewe sasa anakuona ni kama uozo. Haitajalisha ukimpa maneno matamu, yakanukia kama marashi mazuri. Kwake yeye, ile harufu mbaya anayoiona kwako, bado ipo na kamwe haitatoka. 

Ni muhimu tukumbuke kuwa mapenzi huwa hayalazimishwi. Yakilazimishwa, mwisho wake unaweza kuwa mbaya ukaja ukajuta bure.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: