Usipime Umuhimu Wa Mtu Kwa Mahitaji Yako

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Binadamu kwa kawaida, tunaishi kwa kusaidiana. Inaweza ikatokea katika maisha yako ukawa na mtu ambaye kwako wewe ni msaada mkubwa. Pengine ni yeye anayekusaidia katika shida zako mbalimbali. Mtu huyo unaweza ukamuona kuwa ni rafiki au ndugu kwa sababu huwa ni kawaida yake kukusaidia siku zote. Kwa kifupi, mtu huyu tunaweza kusema kuwa ni mkombozi wako kwa kila hali. 

Kuna dada mmoja ambaye alikuwa na mazoea sana na mimi kiasi kwamba, kama akipata shida yoyote, huja kwangu bila wasiwasi wowote. Ikatokea siku moja alikuja kwangu lakini siku hiyo mimi sikuwa na nia ya kumtimizia matakwa yake. Hii ilitokana na sababu kwamba, alikuwa msumbufu sana wakati wa kurudisha. Kwa hali hiyo nilifikia mahali nikawa nimechoka. Kwa uwazi kabisa, nilimwambia kuwa sitaweza kumsaidia safari hii. Aliondoka akiwa na kinyongo moyoni mwake. 

Matokeo yake, alianza kunitangaza kuwa, kwanza sina chochote na wala sifai kwa lolote. Kisa tu eti nimekataa kumsaidia siku hiyo. Alianza kuniona kuwa sina umuhimu tena kwake. Alinisemea ovyo sana kwa watu. Lakini kwa waliokuwa wanamjua, na jinsi nilivyokuwa namsaidia mara kwa mara, walimuona hana shukurani. Waliweza kumwambia machoni pake kuwa hana fadhila na kwamba hakumbuki alikotoka. 

Usemi huu unatuasa tusipime umuhimu wa mtu kwa shida zetu. Ilikuwa ni dhahiri kabisa umuhimu wangu kwa dada huyu ulionekana kwake pale tu nilipokuwa namsaidia. Bila hivyo, bila kumpa misaada, alinigeuza kuwa mimi si lolote wala chochote kwake. Hiyo siyo sahihi hata kidogo. Umuhimu wa mtu haupimwi kwa misaada ama ufadhili anaokupatia. Tujifunze kuwa na shukrani kama binadamu kwani tunahitajiana. Kila mmoja wetu ana umuhimu wake.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: